Ijumaa 18 Aprili 2025 - 09:55
Kwa ajili ya kuokoka na adui hatari (Shetani), hakuna njia nyingine isipokuwa dhikri ya daima

Hawza/ Hadhrat Ayatollah Jawadi Amuli amesema: "Isti‘ādha ya kweli ni hii: kwamba baada ya wasiwasi wa Shetani, roho zetu zielekee kwa Mwenyezi Mungu; kama ambavyo wakati wametangaza hatari na wakasema: 'Nendeni kwenye hifadhi', ni kama kutamka jumla isemayo "Mimi ninakwenda kwenye hifadhi" haitatatuwa tatizo, bali ni lazima kuelekea kwenye hifadhi na kukaa humo."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Jawadi Amuli katika maandiko yake alizungumzia maana ya "isti‘ādha ya kweli" na akasema:

"Kwa ajili ya kuokoka na adui huyu hatari (Shetani), hakuna njia nyingine isipokuwa dhikri ya daima; kama ambavyo ni lazima kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndani ya nafsi na katika siri, kwa kilio na unyenyekevu: «وَاذْکُرْ رَبَّکَ فِی نَفْسِکَ تَضَرُّعًا وَخِیفَةً» (Na mtaje Mola wako ndani ya nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu).
Ni lazima tumtambue Shetani kuwa ni adui, tumpige mawe na kila anapokuja kwetu tujitahidi kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ni rafiki yetu, na Shetani ni adui yetu, na ametupa ahadi ya kututetea:
{إِنَّ اللَّهَ یُدَافِعُ عَنِ الَّذِینَ آمَنُوا} (Hakika Mwenyezi Mungu anawapigania wale walioamini). Anasema: mara tu Shetani anaposhambulia na kutaka kuwahadaa, kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu:
 «وَإِمَّا یَنْزَغَنَّکَ مِنَ الشَّیْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ»  (Na iwapo Shetani atakutia wasiwasi wowote, basi mtafute hifadha kwa Mwenyezi Mungu). Na makusudio ya kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu na isti‘ādha, siyo tu kusema 'A‘ūdhu billāhi min ash-shayṭān ir-rajīm'; isti‘ādha ya kweli ni hii: kwamba baada ya wasiwasi wa Shetani, roho zetu zielekee kwa Mwenyezi Mungu; kama ambavyo wakati ambapo hatari inatangazwa na wakasema: 'Nendeni kwenye hifadhi', basi kusema tu sentensi ya 'Ninakwenda kwenye hifadhi' haitatatuwa suluhisho, bali ni lazima kuelekea kwenye hifadhi na kukaa humo."

Tasnīm, Juzuu ya 3, uk. 399

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha