Jumatano 26 Machi 2025 - 23:27
Siku ya Quds ni siku ya kutangaza mshikamano wa waislamu dhidi ya uhalifu unaofanywa na utawala wa kizayuni

Ayatollah Nouri Hamadani katika ujumbe wake kuhusu Siku ya Quds aliiomba jamii ya waislamu duniani kuonyesha mshikamano wao na umoja dhidi ya uhalifu unaofanywa na utawala wa kinyama wa Kizayuni na mabwana zao.

Kulingana na ripoti kutoka Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Ayatollah Nouri Hamadani kuhusiana na Siku ya Quds ni kama ifuatavyo:

Bismillah Rahman Rahiim
Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kulingana na maelekezo ya Imam alietangulia (r.a), ni Siku ya Quds ya Kidunia, ambayo kwa maono haya na uamuzi wa busara, wenye kudhulumiwa Duniani kote wanatangaza kuuchukia utawala haramu wa kizayuni.
Mwaka huu pia, uhalifu uliofanywa na utawala huu haramu umefikia kiwango cha juu zaidi na kwa kimya kilichooneshwa na mashirika ya kimataifa na kutochukua kwao hatua stahiki, kumeonesha kwamba wanashiriki katika kuharibu na kuua hasa watoto wasio na hatia.

Insha'Allah, kwa mara nyengine, umma wa kiislamu duniani utaonyesha umoja na mshikamano wao dhidi ya uhalifu unaofanywa na utawala huu katili na mabwana zao na kutangaza chuki dhidi yao waziwazi.

Hussain Nouri Hamadani
5 Farvardin

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha