Jumatano 26 Machi 2025 - 23:24
Siku ya Quds, ni siku ya kuufufua umma wa Kiislamu na kuonyesha nguvu ya umma mmoja

Watu wa Palestina waliokandamizwa kwa ajili ya uhuru wa Quds tukufu na ardhi zao za asili, wamepigania kwa umaskini na upweke kwa miaka mingi, na leo hii licha ya usaliti na kukosa ushirika kutoka katika baadhi ya nchi za kiislamu, hali ya kudhoofika na kushuka kwa utawala wa kifisadi wa Wazayuni imeongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Shirika la Habari la Hawza, maelezezo yaliyo tolewa na J'amiatul-Mudarisin kuhusiana Siku ya Kimataifa ya Quds ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Siku ya Kimataifa ya Quds katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni kumbukumbu ya kimkakati na ya kudumu ya Imam wetu mpendwa, na siku hii ina mchango mkubwa katika kuendelea kuwepo na kutosahaulika kwa suala la Palestina kama suala kuu na la msingi katika Dunia ya kiislamu.

Nchi ya kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono watu wa Palestina waliokandamizwa, ilizingatia wosia wa Amirul Mu’minin Ali (a.s) pale aliposema: “Kuweni adui kwa dhalimu na msaada kwa mwenye kudhulumiwa,” na ilijitahidi katika kuonyesha utambulisho wake wa kiislamu na kwa hiyo, Palestina na Quds tukufu bado ni suala kuu na la msingi katika Dunia ya kiislamu.

Watu wa Palestina waliokandamizwa kwa ajili ya uhuru wa Quds tukufu na ardhi zao za asili, wamepigania kwa umaskini na upweke kwa miaka mingi, na leo hii licha ya usaliti na kukosa ushirika kutoka katika baadhi ya nchi za kiislamu, hali ya kudhoofika na kushuka kwa utawala wa kifisadi wa Wazayuni imeongezeka.

Hamasa kubwa ya tufani ya Al-Aqsa imeonyesha kuwa mapigano ya imani na subira ni chanzo cha nguvu na Muqawama baada ya tufani ya Al-Aqsa, imeweza kubadilisha mlingano wa nguvu na mamlaka dhidi ya Israel, uhalifu uliopetuka wa wazayuni wakati wa vita ya hivi vya karibuni Ghaza, Palestina na Lebanon, umeonesha ni wa utawala wa kimabavu na kifisadi kwa kila mtu, na ulimwengu umeona kwa macho yake kwamba Israel, inachukua kisasi cha madhaifu yake katika viwanja vya vita kwenye kuua watoto mauaji ya kimbari, na uharibifu wa hospitali na shule.

Miaka mingi ya mazungumzo na mipango ya makubaliano, si kwamba tu haijafanikiwa kurudisha haki kwa watu wa Palestina waliokandamizwa, bali imemfanya utawala wa kinyama wa wazayuni kuwa na ujasiri zaidi katika mauaji na kumwaga damu, leo umma wa kiislamu wapigania uhuru, na wanazuoni wa dunia pia wamefikia hitimisho kwamba suluhu ya suala la Palestina ni kuupa nguvu muqawama katika ulimwengu wa kiislamu na kuzidisha mapambano dhidi ya utawala wa kifisadi na wale wanao wakingia kifua, kwa hakika kupigana Jihadi kwa Hamas, kutamfanya adui kurudi nyuma na kuelekea kwenye kudhoofika na siku moja njia ya Quds itakuja kufunguliwa kutoka kwenye mapambano.

Jaamiatul-Mudarisin inaheshimu majina na kumbukumbu ya mashahidi wakubwa waliopata shahada katika njia ya uhuru wa Quds nchini Iran, Lebanon na Palestina, hususan mashahidi mashuhuri Haj Qassem Suleimani, Sayyid Hassan Nasrallah, Sayyid Hashim Safiyuddin, Dr. Ismail Hania, Yahya Sinwar na makamanda na wapiganaji wengine na kusema:

Damu za mashahidi hawa zitazidisha nguvu na ukubwa wa Muqawama na wapiganaji wa Muqawama wa kiislamu, wataimarisha dhamira yao ya kuiangamiza Israel.

Mipango ya kishetani ya Trump kuhusu Ghaza na Palestina, haitafaulu na ulimwengu utasimama mbele ya udhalilishaji huu na tamaa zisizo na kikomo.

Siku ya Quds, ni siku ya kuufufua umma wa kiislamu na kuonyesha nguvu ya umma mmoja wa Kiislamu. Ushiriki wa shauku na kishujaa wa watu mashujaa wa Iran, hususan vijana katika maandamano ya siku ya kimataifa ya Quds, ni kuonyesha msaada kwa watu wa Palestina waliokandamizwa na kuhuisha kiaga na Imaam alie tangulia kwa kuendeleza njia ya mapambano dhidi ya utawala wa dhalimu wa kizayuni.

Tunatarajia wananchi wote watajiunga kikamilifu katika siku hii ya kimataifa na tena wataonyesha msaada wao kwa Muqawama wa kiislamu wa Palestina na kutangaza utayari wao kusaidia wapiganaji wa Palestina. Hakika hatua thabiti za waumini waliokua na roho ya uchaji Mungu katika siku hii ni vita vikubwa dhidi ya Israel.

J'amiatul-Mudarisin Qum.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha