Ijumaa 21 Machi 2025 - 17:32
Maelfu ya Wapalestina watekeleza Swala ya Ijumaa licha ya vizuizi vya Israel

Takriban Wapalestina 80,000 wameswali Swala ya Ijumaa ya tatu ya mwezi wa Ramadhani hii leo katika Msikiti wa Al-Aqsa huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, licha ya vikwazo vya Israel na vituo vya ukaguzi kuwazuia maelfu ya waumini wengine kufika eneo hilo takatifu.

Shirika la Habari la Hawza - Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wakfu wa Kiislamu mjini Al Quds, Sheikh Azzam al-Khatib, ameliambia Shirika la Anadolu kwamba waumini 80,000 leo wameshiriki Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Maelfu ya Waislamu walianza kuwasili katika Msikiti wa Al-Aqsa jana Alkhamisi, licha ya mvua kubwa kunyesha na vizuizi vya Israel. Mamia ya waumini walifanya Itikafu msikitini nyakati za usiku sambamba na kuanza kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Kwa Ijumaa ya tatu sasa tangu kuanza mwezi wa Ramadhani, polisi wa Israel wametumwa kwa wingi kwenye lango la Mji Mkongwe wa Quds, unaojumuisha msikiti huo, na katika mitaa na maeneo yanayozunguka msikiti huo.

Baada ya kuhitimishwa Swala ya Ijumaa, waumini walitapakaa katika viwanja vya msikiti na kumbi za ibada kwa ajili ya kusoma Qur'ani na kushiriki katika duru na vikao vya kupata maarifa na elimu. 

Chanzo: parstoday

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha