Jumatano 26 Februari 2025 - 16:06
Dhambi ya mtu binafsi hupelekea ufisadi katika jamii na kuathiri jamii kama sumu na kuharibu uaminifu

Mbali na athari zake za wazi, dhambi zingine zina madhara yaliyofichikana na yenye uharibifu ambapo huathiri ubora wa maisha na baraka za ki_Mungu.

Shirika la Habari la Hawza - Bila shaka, ubaya wowote huathiri hali ya (Jamii), na kwa njia hiyo huathiri hali ya (mtu mmoja mmoja), na husababisha aina fulani ya uharibifu katika mfumo wa kijamii, dhambi na uvunjaji wa sheria ni kama chakula kisicho na afya na chenye sumu, ambacho kitakuwa na athari mbaya kwa mfumo wa mwili wa Mwanadamu, sawa sawa tuwe tunataka au la, hilo litaleta athari mbaya zisizotakiwa, Mwanadamu atapata majibu na athari za asili za hilo.

"Uongo" huharibu uaminifu.

"Usaliti - Khiana - katika Uaminifu / Amana" huvuruga mahusiano ya kijamii.

"Ukandamizaji / Dhulma" daima ni chanzo cha dhulma / ukandamizaji mwingine.

"Matumizi mabaya ya uhuru" husababisha udikteta, na udikteta hupeleka kuleta mlipuko.

"Kuziacha Haki za wanyonge / wasiojiweza" hujenga chuki na uadui, na mkusanyiko wa chuki na uadui unatikisa msingi wa jamii.

Kwa ufupi, kila dhulma, iwe kwa kiwango kidogo au kikubwa, ina athari mbaya, na moja ya tafsiri za Aya inasema: (Nchi kavu na Bahari vyote vitaharibika - Vitapatwa na ufisadi mkubwa - , na hilo linatokea pindi madhambi yanapoongezeka);

«ظَهَرَ الْفَسادُ فِی الْبَرِّ وَ الْبَحْرِ بِما کَسَبَتْ أَیْدِی النّاسِ».

Iko hivyo. (Na huo ndio uhusiano wa asili uliopo kati ya "dhambi" na "ufisadi").(1)

Lakini tunafaidika na riwaya za Kiislamu kuwa: Dhambi nyingi, pamoja na hizi (zilizotajwa hapo juu), huleta mfululizo wa athari mbaya, ambapo uhusiano na mafungano na athari hizo (upo), ingawa kwa mtazamo wa asili, (uhusiano huo) haujulikani.

Kwa mfano, imetajwa katika riwaya kwamba "Kukata Udugu" kunafupisha maisha, na "Kula vitu vilivyoharamishwa" huutia giza moyo (wa Mwanadamu), na "Kuenea kwa uzinzi" husababisha maangamizi kwa watu na kupunguza riziki, nk.

Tunasoma pia katika riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Sadiq (amani iwe juu yake):

«مَنْ یَمُوتُ بِالذُّنُوبِ أَکْثَرُ مِمَّنْ یَمُوتُ بِالآجَالِ».

(Wale wanaokufa kwa sababu ya dhambi ni - wengi mno na - zaidi ya wale wanaokufa kifo cha kawaida) (2).

Maana hiyo hiyo imetolewa katika tafsiri nyingine ndani ya Qur’an Tukufu, pale inaposema:

«وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُری آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنا عَلَیْهِمْ بَرَکات مِنَ السَّماءِ وَالأَرْضِ وَلکِنْ کَذَّبُوا فَأَخَذْناهُمْ بِما کانُوا یَکْسِبُونَ»

((Ikiwa watu wa vijijini na mijini wataamini na wakamcha Mungu, tutawafungulia neema za mbingu na ardhi, lakini walizikadhibisha Aya zetu, na tukawaadhibu (adhabu kali) kwa sababu ya vitendo vyao). (3).

Kwa njia hii, “ufisadi” una maana ya jumla inayojumuisha ufisadi wa kijamii, mabalaa, na kunyimwa / kupokinywa neema (na baraka) .

(1). Surah al_Rum, Aya ya 41.

(2). "Safina al-Bihar", mada ya dhambi.

(3). Surah al_A'raf, Aya ya 96.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha