Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, mjadala kuhusu kurejea waumini duniani, pamoja na kuwa na upande wa kiitikadi, unahusiana pia na uhusiano kati ya kifo, kuendelea maisha ya kiimani na nafasi ya waumini katika kutekeleza malengo na matarajio ya zama za kudhihiri Imam Mahdi (ajf).
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ridha Muhammadi Shahroudi, katika kujibu swali kuhusu iwapo waumini wote wana uwezekano wa kurejea duniani, ameeleza nafasi ya mashahidi na waumini katika mafundisho ya Raj‘ah.
Swali:
Je, waumini wote wana uwezekano wa kurejea duniani kupitia Raj‘ah?
Jibu la Hujjatul-Islam Ridha Muhammadi Shahroudi:
Katika kujibu swali kuhusu iwapo waumini wote wana uwezekano wa kurejea duniani kupitia Raj‘ah, kwanza tunapaswa kusema kwamba msingi wa itikadi ya «Raj‘ah» ni miongoni mwa itikadi zisizopingika katika misingi ya imani ya madhehebu ya Shia. Hii ni kwa sababu riwaya zinazohusiana na suala hilo zimefikia kiwango cha Tawatur, na Aya za Qur’ani Tukufu pia zinathibitisha itikadi hiyo.
Vilevile, kurejea duniani Maimamu (as), hususan Imam Hussein (as), Amirul-Muuminina (as) na Maimamu wengine (as), ni miongoni mwa mambo yaliyothibiti kupitia riwaya za kiwango cha Tawatur, ambazo zimezidi kiwango hicho. Hata hivyo, mijadala mingine inayohusiana na Raj‘ah haijafikia kiwango hicho cha Tawatur, ingawa kuna riwaya zinazozungumzia masuala hayo.
Kwa mfano, baadhi ya riwaya zinasema kwamba iwapo Muumini atafariki kwa kifo cha kawaida, katika kipindi cha Raj‘ah atarejea duniani ili kupata daraja ya kuuawa kishahidi, na iwapo atafariki kwa kuuawa kkshahidi, atarejea ili kuonja kifo cha kawaida.
Vilevile, katika riwaya imeelezwa kwamba Raj‘ah inawahusu waumini wa kweli kabisa na viongozi wakuu wa ukafiri na unafiki.
Kwa mfano, kuhusu mtu anayesoma Dua ya Ahdi kwa muda wa siku arobaini, imenukuliwa kwamba katika kipindi cha Raj‘ah atarejea duniani na atakuwa miongoni mwa wasaidizi wa Imam wa Zama (ajf). Ikiwa mtu huyo atafariki dunia kabla ya kudhihiri Imam wa Zama (ajf), basi atarejea tena duniani katika kipindi cha Raj‘ah.
Riwaya hizi, kwa upande wa mlolongo wa wapokezi wake (Sanad), ni zenye kuaminika na sahihi. Hata hivyo, zinahesabiwa kuwa ni Khabar Wahid, yaani riwaya zisizofikia kiwango cha Tawatur. Kwa hiyo, haiwezekani kuzungumzia maelezo yake ya kina kwa uhakika wa asilimia mia moja.
Ukweli ni kwamba, kwa mujibu wa riwaya, Muumini atapata fursa ya kurejea duniani kupitia Raj‘ah, awe aliuawa koshahidi, alifariki kwa kifo cha kawaida, au alifariki kutokana na tukio kama ajali ya gari.
Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, shahidi atarejea duniani ili hatimaye afariki kifo cha kawaida, huku mtu aliyefariki kifo cha kawaida atarejea duniani ili naye aweze kufikia daraja ya shahada.
Maoni yako