Jumatatu 23 Novemba 2026 - 07:25
Ayatullah Arafi akutana na Ayatullah al-Udhma Makarim Shirazi

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-Udhma Makarim Shirazi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, siku ya Jumamosi, tarehe 30 Aban 1405, amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah al-Udhma Makarim Shirazi, miongoni mwa Mara'ji' wakubwa wa Taqlidi.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Ayatullah Arafi aliwasilisha ripoti kuhusu mipango, shughuli za mageuzi na hali ya Hawza nchini Iran.

Kwa upande wake, Ayatullah al-Udhma Makarim Shirazi, baada ya kusikiliza ripoti iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, alitoa mwongozo na nasaha mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha