Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra) amejibu swali la Istiftaa lililowasilishwa kwake kuhusu suala la «kulipa Kitako cha Tashahudi kilichosahaulika». Jibu hilo linawasilishwa hapa kwa ajili ya wasomaji na watu wote wenye hamu ya kulifahamu.
Kulipa Kitako chaTashahudi Kilichosahaulika
Swali:
Ikiwa mtu atasahau kusoma Tashahudi, na hata baada ya kumaliza Swala akasahau pia kuitekeleza kama Tashahudi ya kulipwa, je, wajibu wake ni upi?
Jawabu:
Wakati wowote utakapokumbuka, kwa mujibu wa tahadhari ya lazima, tekeleza Tashahudi hiyo (ukiwa na udhu na umeelekea upande wa Qibla), kisha tekeleza sijda mbili za kusahau (Sajdatay al-Sahw), kwa kufanya hivyo, Swala yako itakuwa sahihi.
Maoni yako