Jumatatu 26 Oktoba 2026 - 06:28
Fahamu Kipimo cha Kuwatambua Wafuasi wa Ahulbayt (as)

Hawza/ Bibi Fatima Zahraa (as) katika Riwaya, anabainisha kipimo maalumu ambapo kupitia kipimo hicho, mtu anaweza kuwafahamu vyema wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Riwaya inanukuliwa kutoka katika kitabu cha Biharul- Anwar, ambapo katika riwaya hiyo Mtukufu Bibi Fa'tima Zahra (s.a.) amesema:

«إِنْ كُنْتَ تَعْمَلُ بِمَا أَمَرْنَاكَ وَتَنْتَهِي عَمَّا زَجَرْنَاكَ عَنْهُ فَأَنْتَ مِنْ شِيعَتِنَا وَإِلَّا فَلَا.»

“Ikiwa utatekeleza yale tunayokuamrisha na kujiepusha na yale tunayokukataza, basi wewe ni miongoni mwa wafuasi wetu (Shia); vinginevyo, basi si miongoni mwao.”

📚 Rejea: Bihār al-Anwār, Juzuu ya 68, Ukurasa wa 155.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha