Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Abdulali Ahmad al-Bayati, mmoja wa masheikh wa makabila ya Iraq, amesema katika mahojiano: Kumbukumbu ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah hufungua tena majeraha na kukumbusha matukio ya umwagaji damu ambayo Umma wa Kiislamu umeyapitia.
Amesisitiza: Shahada, licha ya maumivu yote inayokuja nayo, bado ni njia kuelekea ushindi. Sisi tuna deni kwenye jihadi ya Sayyid Hassan Nasrullah na tutabaki waaminifu kwenye ahadi yetu, Sayyid Nasrullah ameacha alama ya kudumu ndani ya Muqawama dhidi ya Marekani na Israel.
Al-Bayati ameongeza kuwa: Masiku hupita, kisha kumbukumbu hii hujirudia; jeraha hufunguka tena na moyo hujawa na huzuni, huku mkanda wa matukio ya siku zile za umwagaji damu na za kuhuzunisha ukirudiwa tena.
Akisisitiza kwamba, maumivu haya hayafuti matumaini ya siku zijazo, amesema: Kwa kiwango kilekile ambacho msiba huu mkubwa unaumiza, pia kuna matumaini ya mustakabali bora; mustakabali ambao kichwa chake ni ushindi, kukomesha utawala huu wa kinyang’anyi na waumini kuifikia faraja.
Maoni yako