Jumapili 27 Septemba 2026 - 06:34
Semina Maalumu ya Mtandaoni Inayohusu Maisha ya Mtume (s.a.w.w) kufanyika

Hawza/ Mtandao wa Kimataifa wa Maarifa ya Ahlul-Bayt (as), kwa kushirikiana na Umoja wa Kimataifa wa Maprofesa na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu umeandaa semina maalumu ya mtandaoni inayohusu maisha na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtandao wa Kimataifa wa Maarifa ya Ahlul-Bayt (as), kwa kushirikiana na Umoja wa Kimataifa wa Maprofesa na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, kwa furaha kubwa, unawatangazia kufanyika semina maalumu ya kielimu mtandaoni, inayohusu maisha, mafundisho na urithi wa Mtume Mtukufu wa Mwenyezi Mungu (saww).

Wahadhiri mashuhuri:
Katika semina hiyo wahadhiri ni:

1- Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Dkt. Haidary Ali Mshele
• Mchambuzi wa masuala ya kijamii na kidini

Mada: Mtume Mtukufu (saww); taa ya uongofu kwa wanadamu katika giza la ujinga na ukosefu wa uadilifu.

2- Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Sheikh: Athumani Suya Msellem
• Mwanafunzi, Shahada ya Uzamivu katika Chuo cha Kimataifa cha Almustafa.

Mada: Mtume Mtukufu (saww); Mwanzilishi wa maadili mema na ubinadamu katika ulimwengu mzima.

Kwa moyo wa dhati, mtandao huo unawaalika watu wote wenye shauku, kushiriki katika kikao hiki maalumu cha kielimu na kunufaika na mitazamo yenye thamani ya watafiti na wataalamu mashuhuri.

Siku na muda wa Semina hiyo:

Tarehe: Leo Jumapili, tarehe 27 Septemba 2026

⏰ Muda:
• Dar es Salaam: 18:30
• Tehran: 19:00

💻 Namna itakavyo fanyika: Mtandaoni kupitia jukwaa la Google Meet

🔗 Kiunganishi cha kikao:
https://meet.google.com/tor-dmhb-exk

Semina Maalumu ya Mtandaoni Inayohusu Maisha ya Mtume (s.a.w.w) kufanyika

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha