Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 3 Mehr 1405, iliyofanyika katika Muswalla wa Quds Qum, alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alitoa ujumbe kwa ajili ya kuanza mwaka wa masomo na akabainisha jukumu muhimu kwa vijana wa kiume na wa kike.
Imam wa Ijumaa wa Qum alisema: Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwa wanafunzi wa shule na vyuo unaonesha taswira ya kizazi ambacho kinapaswa kujiandaa kwa ajili ya kuijenga Iran. Ni kizazi ambacho kinapaswa kujijenga, kujifunza elimu, kusogeza mbele mipaka ya elimu, kuhifadhi utambulisho wake na kuchukua nafasi katika maendeleo ya nchi yake.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatima Ma’suma (s.a.) alisema: Kwa mtazamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi, elimu huwa na mamlaka pale inapofuatana na maadili. Katika zama ambazo unyama wa mfumo wa kutawala, hususan serikali ya kihalifu ya Marekani na utawala bandia wa Kizayuni, umeenea, nguvu inayotokana na maadili ni kama ngao ya chuma na upanga mkali unaozuia mikono ya wavamizi dhidi ya wanadamu. Kwa mtazamo wa Uislamu, elimu bila maadili ina thamani ndogo na ni hatari, lakini elimu inapofuatana na maadili huzalisha nguvu yenye uwezo wa kuzuia uovu na kujenga.
Kusifu misimamo ya Rais katika Umoja wa Mataifa
Akirejelea hotuba ya Rais katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema: Hotuba yake ilikuwa mchanganyiko wa mantiki ya kisiasa, utetezi wa haki na kueleza misimamo ya taifa ambalo kwa miaka mingi limebeba gharama ya kusimama dhidi ya uonevu wa madola makubwa, lakini halikuwahi kuinamisha kichwa. Wakati Trump alipoiita Iran kuwa ni ya gaidi, Rais wa Iran, hakutosheka na hotuba iliyokuwa imeandaliwa hapo awali, bali aliibadilisha hotuba yake kutoka katika hotuba ya kawaida ya kidiplomasia na kuifanya kuwa utetezi wa kimaadili na wenye kuelimisha. Kwa kutumia ushahidi na nyaraka, hususan picha ya Imam Shahidi, alieleza kwamba sisi si magaidi, bali ni wahanga wa ugaidi.
Ayatullah Saeedi alisema: Rais alisema katika sentensi fupi na yenye nguvu kwamba: Bomu la atomiki liko Israel, lakini wakaguzi wako Iran, sehemu hii ilivutia sana ulimwengu na wananchi wa Iran, hotuba ya Bw. Pezeshkian haikuwa tu maandishi ya kisiasa, bali ilikuwa simulizi ya taifa ambalo limejeruhiwa, lakini wakati huo huo linasisitiza juu ya upinzani na kusimama imara.
Wananchi wanapaswa kupinga kwa ajili ya kuilinda Iran
Imam wa Ijumaa wa Qum, katika kuadhimisha Wiki ya Ulinzi Mtakatifu, alisema: Ulinzi Mtakatifu ni uzoefu hai wa kuielewa leo na kujenga kesho. Vita vya kulazimishwa vya leo vimeonesha kwamba bado tuko katikati ya njia kubwa, kuanzia katika vita vya kulazimishwa vya miaka minane hadi vita vya kulazimishwa vya hivi karibuni, imeonekana kwamba ingawa adui na zana zimebadilika, jambo hili limebaki kuwa lilelile: Taifa la Iran linapaswa kuendelea kupinga kwa ajili ya kuilinda Iran, uhuru wake na heshima yake.
Vita bado havijaisha
Aliendelea kusema: Hii ina maana kwamba vita bado havijaisha, ingawa uwanja na mbinu zake zimebadilika, njama na chuki ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na upinzani wa wananchi, ambao kwa zaidi ya usiku 200 wamekuwa mitaani, vinaendelea. Kwa sababu hiyo, kwa kaulimbiu ya Kihusayni ya «هیهات مناالذله» (Uwe mbali nasi udhalili), tunapaswa kupambana na adui katika nyanja zote na kwenye ngome zote na kumuangusha.
Kuvua hijabu ni haramu ya kisheria ya kidini na kisiasa
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qum aliongeza: Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi alisema kuhusiana na kuvua hijabu kwamba kuvua hijabu ni haramu ya kisheria, kidini na kisiasa. Maana ya uharamu wa kisiasa ni kwamba katika mazingira ya sasa, suala la kuvua hijabu si dhambi ya mtu binafsi pekee, kwa sababu limegeuzwa kuwa chombo cha fitina na ufisadi mikononi mwa maadui, chombo cha kudhoofisha usalama wa taifa na chombo cha kuupindua mfumo.
Alikumbusha kuwa: Kwa sababu hiyo, wale ambao bila ya kujua wanavua hijabu kutokana na njama za maadui, wanapaswa kuelimishwa kwa njia sahihi na kukumbushwa juu ya hatari ya adui, lakini wale wanaovua hijabu kwa kujua, wanaohatarisha usalama wa taifa na ambao wamekuwa chombo mikononi mwa maadui, wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.
Pole kkufuatia kufariki Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani
Mwakilishi wa Waliyy al-Faqih Qum alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alitoa ujumbe kufuatia kufariki Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani, akatoa salamu za rambirambi kwa Hawza, wanafunzi wake na familia yake, na akataja baadhi ya sifa za mwanazuoni huyo. Alisema: “Mwanazuoni huyu mkubwa alitumia maisha yake yote, isipokuwa miaka michache ya mwanzo ya utoto wake, katika njia ya kujifunza, kufundisha na kufanya utafiti; na daima alichukuliwa na watu wa rika lake, walioishi katika zama zake, pamoja na walimu wake, kuwa ni mtu mtafiti na mwenye mtazamo wa kina.”
Muqawama ndio njia pekee
Akirejelea kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah, alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, katika ujumbe wake wa kutoa rambirambi kwa ajili ya kuuawa kishahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, alisema kwamba; Sayyid wa Muqawama hakuwa mtu binafsi tu, bali alikuwa njia na shule, na njia hiyo itaendelea. Kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ilikuwa yenye kutuliza huzuni, na pia ilikuwa bishara ya kuendelea kwa jukumu lake kupitia Katibu Mkuu anayefuata wa Hizbullah ya Lebanon. Sheikh Naim Qassem pia katika ujumbe wake kwa Mkutano wa Shahidi wa Muqawama alisema kwamba muqawama ndio njia pekee ya kuikomboa ardhi, na njia nyingine ni kupoteza muda. Huko Lebanon, tumeshajaribu moja kwa moja chaguo la muqawama, na chaguo hili huikomboa ardhi na mwanadamu.
Maoni yako