Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kufika kumbukumbu ya mwaka wa kuuawa kishahidi Mwanamapambano Shahidi, Sayyidush-Shuhadaa wa Muqawama, Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), kazi tatu mpya zinazomlenga shahidi huyo mkuu, katika upande wa utu wake, fikra, jihadi na urithi wake wa vyombo vya habari, zinazinduliwa kwa juhudi za Taasisi ya Kimataifa ya Amirul-Muuminina (as).
Kila moja ya kazi hizi tatu, kwa mtazamo wake tofauti, inashughulikia upya vipengele na sifa za utu, fikra, jihadi na shughuli za Sayyidush-Shuhadaa wa Muqawama za vyombo vya habari; vipengele ambavyo vinapounganishwa pamoja vinachora sura ya mwanamapambano mwenye mfumo na mkondo maalumu wa fikra, ambaye aliunganisha fikra, jihadi na ujumbe wa vyombo vya habari ndani ya uwanja wa Muqawama.

“Shahidu al-Aqdas”; simulizi kutoka katika uwanja wa jihadi
Kazi ya kwanza yenye jina “Shahidu al-Aqdas”, ni simulizi kwa lugha ya Kifarsi kutoka kwa Kamanda Abdulamir Afrawi, anayejulikana kwa jina la “Abu Hadi”, kuhusu kumbukumbu na simulizi zake juu ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah. Kazi hii, kwa kutegemea mazungumzo na kumbukumbu za kihistoria, inatoa upya sehemu ya mwenendo, utu na uzoefu wa kijihadi wa Sayyidush-Shuhadaa wa Muqawama, kwa mtazamo wa mmoja wa watu waliokuwa pamoja naye na wapiganaji wenzake, na inatoa picha iliyo karibu zaidi ya utu na mwenendo wa kijihadi wa shahidi huyo.
“Qawafi an-Nasr”; ushairi unaosimulia msiba wa Sayyid wa Muqawama
Kazi ya pili ni mkusanyiko wa mashairi ya Kiarabu wenye jina “Qawafi an-Nasr”, wenye zaidi ya kurasa 400 na karibu kaswida 150, uliotengwa kwa ajili ya kumlilia na kumsifu Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah.
Katika mkusanyiko huu, washairi kutoka nchi za Iran, Iraq, Lebanon, Syria, Yemen, Bahrain, Oman na Tunisia, kila mmoja kwa lugha ya ushairi, amesimulia sehemu ya utu, jihadi, shahada na nafasi ya Sayyidush-Shuhadaa wa Muqawama. Mkusanyiko huu, uliokusanywa na Dkt. Ali Afrawi, unatoa picha ya mwitikio wa kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah katika ushairi wa kisasa wa Kiarabu, pamoja na muunganiko wa hisia, ushujaa na Muqawama katika fasihi ya eneo hili.
“Maktaba ya Nasrillah”; kuisoma upya dhamira ya vyombo vya habari
Kazi ya tatu yenye jina “Maktaba ya Nasrallah”, imejikita katika kuisoma upya fikra na dhamira ya vyombo vya habari ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, na inajumuisha ufafanuzi wa barua ya kihistoria ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah kwa Mtandao wa Kimataifa wa Al-Ahwaz, pamoja na mahojiano ya kihistoria yaliyofanywa na shahidi huyo.
Mwanzoni mwa kazi hii kuna utangulizi na kumbukumbu za Hujjatul-Islam wal-Muslimin Payman Alinajad, Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Amirul-Muuminina (as), kuhusu kukutana kwake na Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah. Baada ya hapo, barua na mazungumzo yake ya kihistoria vimechambuliwa upya kwa mtazamo wa dhamira ya vyombo vya habari katika uwanja wa jihadi ya kifikra, kiutamaduni na ya kubainisha ukweli.
Kazi hii inajitahidi, kwa kutegemea kauli na mtazamo wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, kulipa umuhimu suala la nafasi ya vyombo vya habari katika uwanja wa Muqawama na ulazima wa kuwepo nguvu na kwa athari katika uwanja wa vita vya simulizi; uwanja ambao kwa mtazamo wake, vyombo vya habari si tu chombo cha kufikisha ujumbe, bali ni sehemu ya uwanja wa jihadi na kuulinda ukweli.
Kazi hizi tatu, “Shahidi al-Aqdas”, “Qawafi an-Nasr” na “Maktaba ya Nasrallah”, kila moja kwa lugha tofauti, zinasimulia sehemu ya urithi ulioachwa na Sayyidush-Shuhadaa wa Muqawama; kuanzia kumbukumbu na uwanja wa jihadi, hadi ushairi na fasihi ya Muqawama na dhamira ya vyombo vya habari.
Jumla ya kazi hizi ni jitihada za kurekodi na kuisoma upya misingi na sifa za utu, fikra, jihadi na shughuli za vyombo vya habari za shahidi ambaye jina na mfumo wake wa fikra vimefungamana na historia ya Muqawama.
Hafla ya uzinduzi wa kazi hizi tatu itafanyika sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kuuawa kishahidi Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah.
Maoni yako