Jumapili 13 Septemba 2026 - 18:00
Mikakati mikuu ya uongozi wa elimu na malezi / Kusisitiza kuhamasishwa uwezo na rasilimali zote kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa elimu na malezi

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, amefafanua mikakati mikuu ya uongozi wa elimu na malezi, huku akisisitiza umuhimu wa kuhamasisha uwezo na rasilimali zote za wananchi na serikali kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa elimu na malezi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A’rafi, Mkuu wa Hawza nchini Iran, katika kufafanua mikakati mikuu ya uongozi wa elimu na malezi, alisisitiza: “Katika kuhuisha huku kukubwa na mawimbi yanayokuja, jukumu la wanasayansi, wasomi, watu wenye vipaji na elimu, taasisi zinazohusika, na hasa taasisi kubwa ya elimu na malezi pamoja na walimu wetu waheshimiwa, ni zito na kubwa sana, na waasisi wa malezi ya Kiislamu wanabeba jukumu kubwa mbele ya kizazi cha sasa, vijana na vizazi vijavyo.”

Kuzitafakari upya changamoto na fursa mpya za mfumo wa elimu na malezi ni jambo jingine ambalo Mkuu huyo wa Hawza amelisisitiza, anaamini kwamba uongozi wa elimu na malezi pamoja na usimamizi wake unaofanywa na familia na mamlaka ya dola, umewekwa katika shabaha ya mashambulizi ya mabadiliko ya kiteknolojia, matukio ya kijamii na utamaduni wa kimaada na Kimagharibi. Katika mfumo wa Kiislamu na kwa kuzingatia mantiki ya Uislamu, mamlaka na uongozi huu lazima ulindwe, na kwa mujibu wa mantiki imara ya Uislamu, huku ikizingatiwa hali na mabadiliko ya zama, lazima uhifadhiwe, ujengwe upya na ubuniwe upya.

Ayatullah A’rafi pia alisisitiza jambo hili la kimkakati kwamba shule ni kitovu cha msingi na mhimili mkuu wa elimu na malezi, na kwamba walimu, wakuu wa shule na walezi ndio viongozi na wasanifu wa malezi. Kila juhudi ya kujenga shule yenye kiwango kinachotarajiwa na kuinua maarifa na uelewa wa walimu na wakuu wa shule ni jukumu la kila mmoja.

Endelea kusoma hapa chini changamoto, fursa na mikakati mikuu ya uongozi wa elimu na malezi, kwa mtazamo wa Ayatullah A’rafi:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kufanyika mkutano wa Kituo cha Malezi ya Kiislamu, kwa ushiriki wa wajumbe waheshimiwa na wadau wa elimu na malezi katika hatua hii nyeti na mpya ya Mapinduzi ya Kiislamu, na katikati ya matukio machungu na matamu ya historia ya Iran na Uislamu, kunaweza kuwa fursa mpya ya kuzitafakari upya changamoto na fursa mpya za mfumo wa elimu na malezi, pamoja na kutafuta suluhisho jipya na lenye manufaa.

Hatua mpya ya Mapinduzi ya Kiislamu imeanza kwa kuuawa kishahidi kiongozi wetu na kiongozi wa Mapinduzi (r.a.) pamoja na mashahidi wetu wapendwa, wanafunzi wadogo wa shule ya Tayibah Minab na mashahidi wa Iran na mhimili wa Muqawama. Hatua hii imefungamana na vita vya tatu na makabiliano ya msingi na ya kistaarabu kati ya fikra na mfumo wa Mapinduzi ya Kiislamu na mhimili wa Muqawama dhidi ya mfumo wa utawala wa kiburi na ubeberu wa Marekani na Israel.

Taifa lililotumwa kwa ajili ya kutekeleza ujumbe na Umma ulioamshwa, kwa msingi wa fikra za Imam Khomeini (r.a.), uongozi wa Imam Shahidi (r.a.) na mrithi wake mwema, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Mwenyezi Mungu amlinde), pamoja na kujitolea vikosi vya kijeshi na vikosi vya kujitolea, na vikosi vya mhimili wa Muqawama, ndio wasanifu wa sura hii mpya, chipukizi hili jipya na mwangaza mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ufufuo huu mkubwa na mawimbi yanayokuja, jukumu la wanasayansi, wasomi, watu wenye elimu na vipaji, taasisi zinazohusika, na hasa taasisi kubwa ya elimu na malezi pamoja na walimu wetu waheshimiwa, ni zito na kubwa sana. Waasisi wa malezi ya Kiislamu mbele ya kizazi cha sasa, vijana na vizazi vijavyo, wanabeba jukumu kubwa. Kituo hicho chenye chemchemi ya uhai, sambamba na taasisi ya Elimu na Malezi, walimu, walezi na wakuu wa shule wenye kujitolea na wenye misimamo ya kimapinduzi, kinaweza kuwa kinara wa mabadiliko yajayo, kutengeneza fursa kubwa na kushinda changamoto zilizopo sasa.

Nikiwa nawasalimu kwa heshima, unyenyekevu, shukrani na pongezi watumishi wote waheshimiwa wa mfumo wa elimu na malezi, wajenzi wa mustakabali wa vizazi vijavyo, pamoja na wote wanaoshiriki katika uwanja huu wenye nuru na washiriki wa kituo hiki na mkutano huu wenye baraka, napenda kukumbusha mambo yafuatayo:

1) Meli ya kuinua na kulea mwanadamu pamoja na mifumo ya elimu na malezi katika zama zetu inakabiliwa na upepo mwingi wa upinzani na mawimbi mengi ya dhoruba. Pamoja na fursa kubwa zilizopo, imezingirwa na changamoto kubwa, baadhi ya changamoto hizo zinaweza kuashiriwwa kama ifuatavyo:

A) Utawala wa fikra za kimaada na kutawala kwa mtazamo usio wa Kiungu katika akili na nafsi ya mwanadamu wa zama hizi, pamoja na kutawala kwa mantiki ya kimaada na isiyo takatifu katika nyanja mbalimbali za maarifa, maisha, elimu na teknolojia, na katika mifumo ya elimu na malezi ya Magharibi na duniani, ni miongoni mwa majanga na madhara makubwa.

Malezi ya mtoto, kijana balehe na kijana katika mazingira kama hayo, yaliyotenganishwa na ulimwengu wa utakatifu na fadhila za kiroho na kimaanawi, yanajengwa katika mazingira hayo, na msingi wa ubinadamu, licha ya mapambo yote ya ustaarabu wa Magharibi na manufaa yake ya nje, unabadilishwa na kupotoshwa; na mwanadamu hupoteza johari safi ya maumbile yake pamoja na maadili yake ya Kiungu na ya kiroho.

B) Pamoja na utawala huo wa kimaada na wa kuzingatia wingi na vipimo vya kidunia, ni lazima pia tuongeze mabadiliko ya kiteknolojia na anga ya mtandao, ambayo yameunda mazingira mengine ya maisha kwa mwanadamu na kijana. Pamoja na manufaa yake mengi yasiyohesabika, yameleta hatari nyingi kwenye fikra, moyo na nafsi ya mwanadamu pamoja na mifumo ya elimu na malezi. Sambamba na hayo, maendeleo ya sayansi za utambuzi na maendeleo ya akili bandia yameweka upeo mgumu na muhimu mbele ya mustakabali wa mwanadamu.

Mabadiliko haya, kwa upande mmoja, yameongeza kasi na usahihi wa mifumo ya utafiti, uchunguzi, kujifunza elimu na kupata ujuzi; lakini kwa upande mwingine, kuhamia katika mazingira ya elimu za kikabila na za mtandaoni na zile zinazotegemea akili bandia kunafanya uhusiano wa kibinadamu na wa karibu, mwingiliano wa wanadamu, pamoja na uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi na fadhila takatifu na za kiroho, kuwa hafifu na kupoteza mwangaza wake. Aidha, kunazuka wasiwasi zaidi kuhusu upeo wa mustakabali.

C) Zaidi ya mambo yaliyotajwa, tunapaswa pia kuashiria mfumo wa kishetani na wa kibeberu wa utawala, pamoja na kutawala mali, nguvu na hila za kisiasa zisizo za haki duniani, na jinsi ulivyoshikilia mifumo na majukwaa ya uundaji wa utamaduni na elimu na malezi duniani.

Nguvu hii ya kishetani imeupanga utamaduni na malezi duniani kwa msingi wa roho ya kiburi, mantiki ya kimaada na mwelekeo wa matamanio ya kimaada, na imezuia mwelekeo wa kibinadamu na wa Kiungu pamoja na mantiki ya uadilifu na kiroho, na kuuweka pembeni.

D) Vilevile, tunapaswa kuashiria mabadiliko mbalimbali ya kisayansi, kiteknolojia na kimaarifa ambayo yamemletea kijana na mwanadamu wa leo fikra mpya, maswali mapya na matakwa mapya. Fikra za kidini, kiroho na za Kiungu zimekabiliwa na masuala na changamoto mpya, na jambo hili ni onyo muhimu; lakini wakati huo huo, ikiwa litakabiliwa kwa usahihi, linaweza kuwa lenye kuleta habari njema na matumaini.

E) Hii ni baadhi ya mifano ya matukio yanayotokea na changamoto za msingi za elimu na malezi. Yote tuliyoyataja na yale ambayo hatukuyataja yamesababisha na yataendelea kusababisha udhaifu wa “uongozi wa elimu na malezi” katika kiwango cha dunia na katika nchi yetu. Jambo hili linaweza kuleta madhara makubwa sana, lina vipengele mbalimbali na changamano, na ni lazima kufanywe tafiti na kuchukuliwa hatua za msingi ili kulitatua.

2) Mambo tuliyoyataja ni sehemu tu ya changamoto za msingi za elimu na malezi katika zama hizi, na yameweka mifumo ya maarifa, sayansi na utamaduni pamoja na mifumo ya elimu na malezi katika Hawzah, vyuo vikuu na taasisi za elimu na malezi katika mazingira ya dhoruba na mawimbi makali.

Inafaa kuzingatiwa kwamba, misimamo ya watendaji wa kisiasa, kitamaduni, kisayansi na kielimu mbele ya mabadiliko haya inatofautiana. Baadhi yao wanaamini na kuyakubali mabadiliko haya ya kimaada na ya kuiga Magharibi, na kutokana na kutokuwa na uelewa wa kina, kwa urahisi hujisalimisha kwa mawimbi haya na mkondo unaotawala. Wengine hawana uelewa wa kina kuhusu matukio haya, lakini wanakabiliana nayo kwa namna ya juu juu na ya nje.

Msimamo sahihi ni kukabiliana na mawimbi haya kwa uelewa, hekima na kwa namna yenye ushiriki wa dhati, pamoja na kuchukua hatua za msingi za kulinda utambulisho wa Kiislamu na wa kiasili na mfumo wa elimu na malezi, bila shaka, njia hii ina changamoto na inahitaji maandalizi makubwa.

3) Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa cheche mpya na kimondo chenye mwangaza katika giza la ulimwengu wa zama hizi, na yaliweka msingi wa mtazamo mpya kuhusu maarifa, roho, uadilifu na maendeleo.

Mapinduzi ya Kiislamu ni mabadiliko yenye matabaka mengi, yenye pande na vipengele mbalimbali, na yenye upeo mpana. Tabaka muhimu zaidi na la kina zaidi ni upande wake wa maarifa na fikra. Kwa hiyo, taasisi ya Elimu na Malezi, na baadaye vyuo vikuu na Hawzah, zinapaswa kuwa kituo, kitovu na uwanja wa kudhihirisha upande huu wa kimaarifa wa Uislamu wetu mtukufu na Mapinduzi ya Kiislamu. Katika suala hili, nafasi ya kipekee na isiyoweza kubadilishwa ya taasisi ya Elimu na Malezi na walimu wetu waheshimiwa, sambamba na familia na vyombo vya habari, ni ya kimkakati na ya kudumu.

4) Katika mapambano dhidi ya mashambulizi ya waja wa shetani wanaoabudu mali, kuachiliwa kwa matamanio na hawaa za kishetani, pamoja na mashambulizi mbalimbali yanayokikabili kizazi cha sasa, kuna ulazima wa kukabiliana na suala la malezi kwa hekima, uwajibikaji, ari, ushiriki hai na msimamo wa kimapinduzi. Miongoni mwa misingi na mambo yote muhimu, kuna mambo kadhaa yenye umuhimu wa pekee ambayo ninayataja:

Kwanza: Uongozi wa elimu na malezi pamoja na usimamizi wake unaofanywa na familia na mamlaka ya dola, umewekwa katika shabaha ya mashambulizi ya mabadiliko ya kiteknolojia, matukio ya kijamii na utamaduni wa kimaada na Kimagharibi. Katika mfumo wa Kiislamu na kwa mujibu wa mantiki ya Uislamu, mamlaka na uongozi huu lazima ulindwe, na kwa kuzingatia mantiki imara ya Uislamu pamoja na hali na mabadiliko ya zama, lazima uhifadhiwe, ujengwe upya na ubuniwe upya.

Pili: Kuimarisha kizazi cha vijana, kuimarisha misingi yao ya kimaarifa na kuimarisha azma zao ni msingi wa malezi katika kipindi hiki chenye misukosuko. Upinzani dhidi ya mawimbi ya mashambulizi unategemea uimara wa azma na kuimarishwa maadili matakatifu na ya juu katika nafsi. Kwa hiyo, mfumo mzima wa elimu unapaswa kuweka uelewa sahihi wa sifa za vizazi vipya katika kilele cha vipaumbele vyake, na kuchunguza na kutekeleza mbinu na njia zinazofaa kwa ajili yake.

Tatu: Hati ya Mabadiliko ya Elimu na Malezi ingeweza kuwa mwanzo wa kuijenga upya na kuiendeleza taasisi ya Elimu na Malezi. Hata hivyo, licha ya baadhi ya hatua na nia nzuri zilizochukuliwa katika kuitekeleza, hatukushuhudia mafanikio yanayofaa katika kiwango kilichotarajiwa. Sababu za jambo hili baadhi yake ziko wazi na nyingine ziko nje ya upeo wa mazungumzo haya, sasa ni lazima kuchukua hatua kwa ajili ya kuitekeleza, pamoja na kuijenga upya na kuikamilisha, azma na dhamira ya jamii ya walimu wenye kujitolea na kuwajibika, pamoja na kudai utekelezaji wake na kushirikiana kwao, vinaweza kuwa na athari kubwa na kusaidia sana.

Nne: Shule ni kitovu cha msingi na mhimili mkuu wa elimu na malezi, na walimu, wakuu wa shule na walezi ndio viongozi na wasanifu wa malezi, kila juhudi ya kujenga shule yenye kiwango kinachotarajiwa na kuinua maarifa na uelewa wa walimu na wakuu wa shule ni jukumu la kila mmoja, bila shaka, sambamba na umuhimu wa kuinua maarifa, uelewa na hali zao za maisha, hadhi yao katika jamii na nafasi ya juu ya taasisi ya Elimu na Malezi pamoja na jamii kubwa na yenye heshima ya walimu na walezi ni mambo yenye umuhimu wa pekee.

Wanapaswa kuthaminiwa na kupewa nafasi ya juu, kwa sababu jukumu na wajibu wao ni mzito sana.

Tano: Kwa ujumla, kizazi cha vijana balehe na vijana wa rika, taasisi ya familia na taasisi ya Elimu na Malezi vinapaswa kuwa katika kilele cha vipaumbele vya taasisi zote za mfumo wa Kiislamu, mihimili ya utekelezaji na utungaji wa sheria, pamoja na jamii nzima. Kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa Elimu na Malezi, ni muhimu kuhamasisha uwezo na rasilimali zote za wananchi, serikali na mamlaka, pamoja na taasisi za kijamii.

Mwishoni, nawashukuru waandaaji, washiriki na wahudhuriaji waheshimiwa wa mkutano huo wa imani na mkutano wa kitamaduni. Ninamuomba Mwenyezi Mungu awape mafanikio wapendwa wote pamoja na kituo hicho chenye chemchemi ya uhai katika kuitumikia dini ya Uislamu, Mapinduzi na nchi ya Kiislamu. Nnahitimisha kwa kuwakumbuka na kuwasalimia Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, hasa Khatamul-Awsiyaa, Hadhrat Waliyyul-Asr, roho zetu ziwe fidia kwake, pamoja na mashahidi wakuu wa Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, hususan Imam Mkuu na Kiongozi Shahidi (r.a.). Kwa unyenyekevu mkubwa, ninamuomba Mwenyezi Mungu Mwenye kutoa neema atupe ushindi wa Uislamu na Waislamu, taifa shupavu la Iran, vikosi vya kijeshi na mhimili wa Muqawama.

وَآخِرُ دَعْوَانَا أَنِ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

Alireza A’rafi
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha