Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Jaafari na mwanazuoni wa Kishia nchini Lebanon, alimtumia Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, barua ya wazi ambayo ilisema: Kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu namwambia Rais Joseph Aoun: Kila kinachotokea katika eneo hili ni hatari sana, na jambo ambalo ni muhimu kwetu kwa mtazamo huu ni Lebanon; kwa sababu historia ya nchi hii ni kubwa kuliko hatua fulani ya kisiasa, au kujifunga kwa upande fulani, au wimbi kubwa la kikanda au kimataifa. Uhalisia wa Lebanon tangu kuanzishwa kwake ni ushahidi kwamba nchi hiyo ina uwezo wa kitaifa wenye muundo changamano ambao haukubali rushwa wala kumtukuza na kumpigia debe yeyote aliye nje ya mfumo wake wa kisiasa na fomula yake ya makubaliano.
Aliongeza kuwa: Ili mambo yawe wazi, namwambia Rais Joseph Aoun: Washington na Tel Aviv haziwezi kuimeza Lebanon; zinaweza kubadilisha Mashariki ya Kati, lakini haziwezi kuibadilisha Lebanon. Kwa mfano, eneo la Venezuela ni kilomita za mraba milioni moja, lakini pamoja na hayo serikali yake ilianguka ndani ya robo saa tu, wakati Tel Aviv, kwa ushiriki wa Washington, NATO na silaha ambazo hazijawahi kuwa na mfano katika historia ya vita vya maamuzi, iliendesha vita kwa miaka mitatu mfululizo kwa lengo la kuimeza Lebanon, kiasi kwamba dunia ilishangazwa na kushindwa kwake kimkakati mbele ya kijiji cha mpakani kusini kinachoitwa “Majdal Zoun”.
Sheikh Qabalan aliendelea kusema: Ushahidi wa jambo hili ni kwamba haipaswi kutegemewa Washington, Tel Aviv na orodha za fitina za kimataifa na kikanda. Historia ya Lebanon katika eneo hili ni ngumu zaidi ya ugumu na chungu zaidi ya uchungu, na suluhisho liko katika kuheshimu muundo wa kitaifa na kupitisha fomula ya makubaliano kwa ajili ya kuiokoa Lebanon, na katika kuepuka kuangukia katika miradi ya fitina za kimadhehebu ambazo hazitasimama katika mpaka wowote. Ni wazi kabisa kwamba Washington na Tel Aviv wanataka kuwadhibiti Mashia, huku kukiwa na mazingira ya “kuifanya Lebanon kuwa ya Kizayuni” na kumaliza kila nguvu yenye mamlaka ya kitaifa inayopingana na mradi wa kuifanya nchi hii kuwa ya Kizayuni.
Aliendelea kusema: Hili ndilo jambo ambalo vita hatari zaidi vya maamuzi katika eneo hili vimeshindwa kabisa kulifikia, na leo Washington inakabiliwa na mgogoro wa tawala yake ya kimkakati ambayo inazikwa katika Mlango wa Hormuz mikononi mwa Tehran. Suluhisho liko katika kulinda maslahi ya familia ya kitaifa yenye mamlaka ya Lebanon, wala si katika kuinyanyasa jamii fulani kwa misingi ya kimadhehebu. Kinachofanywa na mamlaka ya utendaji ni miradi ya mauaji ya kimbari inayolenga kundi moja maalumu pekee, ilhali jamii hiyo hiyo ndiyo iliyoiikomboa Lebanon siku ambayo Israel ya kigaidi ilipokuwa imeikalia kwa mabavu, na ndiyo iliyopambana na miradi yote ya kugawanya nchi ili kuhifadhi fomula ya kitaifa. Na jamii hiyo hiyo leo inaongoza nguvu kubwa zaidi ya kitaifa yenye mamlaka inayoilinda Lebanon na uwepo wake, na kwa njia hii inalinda nchi, serikali, taasisi za umma na vyombo mbalimbali, huku macho yake yakiwa yameelekezwa katika kuulinda mradi wa kitaifa na kile kinachomaanishwa na ujenzi huu wa kihistoria wa msingi wa taifa.
Maoni yako