Jumamosi 1 Agosti 2026 - 14:43
Zaidi ya mazuwari milioni 3 wameingia Iraq hadi sasa kwa ajili ya Arubaini

Hawza/ Mkuu wa Kamati ya Habari ya Usalama ya Iraq ametangaza kuwa idadi ya mazuwari walioingia Iraq kupitia mipaka mbalimbali kwa ajili ya kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as) imevuka watu milioni 3 na laki 435.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Meja Jenerali Saad Maan, Mkuu wa Kamati ya Habari ya Usalama ya Iraq, leo Ijumaa alitangaza kuwa idadi ya mazuwari walioingia Iraq kupitia mipaka mbalimbali kwa ajili ya kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (as) imezidi watu milioni 3,435,000.

Aliongeza kuwa; mazuwari hao wametoka katika mataifa 172 tofauti kwa ajili ya kushiriki katika ibada ya ziara ya Arubaini. Akisisitiza kuwa ziara hiyo inaendelea kwa utaratibu mzuri, urahisi mkubwa na nidhamu ya hali ya juu, alisema kuwa; vikosi vya usalama pamoja na mawakibu za Husseini vinaendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana na mazingira bora yanaandaliwa kwa ajili ya mazuwari.

Aidha, alibainisha kuwa mipango maalumu ya kiusalama na ya huduma kwa ajili ya ziara hii bado inaendelea kutekelezwa, kwa lengo la kuhakikisha mazuwari wanapata urahisi wa kusafiri na kutembea katika maeneo mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha