Alhamisi 30 Julai 2026 - 19:18
Lengo la Marekani na Saudi Arabia kuivamia Iraq ni kuzuia utulivu wa nchi hiyo

Hawza/ Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq limelaani vikali uvamizi wa Marekani na Saudi Arabia dhidi ya ardhi ya Iraq na kusema kuwa; lengo la hatua hiyo ni kuzuia utulivu wa Iraq na kukwamisha juhudi za kuujenga upya uchumi wake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq limelaani vikali uvamizi wa Marekani na Saudi Arabia dhidi ya ardhi ya Iraq na kusema kuwa; lengo la hatua hiyo ni kuzuia utulivu wa Iraq na kukwamisha juhudi za kuujenga upya uchumi wake.

Ali Fadhil Al-Difa'i, msemaji rasmi wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq, alisema: "Tunalaani kwa nguvu uvamizi wa Marekani na Saudi Arabia dhidi ya Iraq pamoja na kulengwa vikosi rasmi vya usalama vya Hashd al-Shaabi, jambo lililosababisha idadi kubwa ya mashahidi na majeruhi. Tunashangazwa sana na ukweli kwamba uvamizi huu umetokea wakati Serikali ya Iraq ilikuwa ikifanya juhudi za dhati za kufungua ukurasa mpya katika uhusiano wake na nchi za Ghuba ya Uajemi; tena siku chache tu baada ya ziara ya Waziri Mkuu nchini Marekani na kutiwa saini hati 48 za makubaliano ya awali (Memorandum of Understanding) kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kuingia katika hatua mpya ya mahusiano."

Aliendelea kusema: "Kilichotokea kinaweza kuwa sehemu ya juhudi za muungano wa Kizayuni na Marekani za kuzuia kufikiwa kwa makubaliano ya pamoja kati ya nchi za eneo hili kuhusu kuamua mustakabali wa usalama na uchumi wao bila kuingiliwa na mataifa ya nje. Aidha, lengo la hatua hii ni kuzuia utulivu nchini Iraq, kukwamisha juhudi za kuujenga upya uchumi wake, na kuzuia kurejea kwa nafasi ya Iraq kama kitovu kinachozikutanisha nchi za eneo hili pamoja na kuwa mpatanishi chanya katika kutatua migogoro na kujenga maelewano kati ya serikali mbalimbali."

Al-Difa'i alisisitiza: "Tunaamini kwamba uvamizi huu hautaweza kudhoofisha azma ya vikosi vya usalama, uthabiti wa wananchi wetu, wala nafasi na mchango wa Iraq. Hatima ya njama zote zinazopangwa dhidi ya mapenzi na irada ya wananchi wetu wakubwa ni kushindwa."

Mwishoni alisema: "Tunamuomba Mwenyezi Mungu Awarehemu mashahidi wetu watoharifu miongoni mwa makamanda wa Hashd al-Shaabi waliokuwa na ujasiri na uzalendo, na Awaponye majeruhi wote uponyaji wa haraka."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha