Jumatatu 27 Julai 2026 - 04:30
Netanyahu hana nafasi mjini London

Hawza/ Meya wa London amesisitiza kwamba Benjamin Netanyahu anapaswa kukamatwa iwapo atasafiri kwenda Uingereza, na ametangaza kuwa atailazimisha serikali kuu ya nchi hiyo kutekeleza hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) dhidi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islami Analysis, matamshi ya Sadiq Khan, Meya wa London, kuhusu ulazima wa kukamatwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, endapo atasafiri kwenda Uingereza, yameibua wimbi jipya la mvutano wa kidiplomasia kati ya London na Tel Aviv.

Sadiq Khan, katika mahojiano na Channel 4 News, akirejelea hati ya kukamatwa Netanyahu iliyotolewa mwezi Novemba mwaka 2024 na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), alisisitiza kwamba; Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anahesabiwa kuwa "mtu asiyetakiwa" (Persona Non Grata) mjini London.

Nitailazimisha Serikali ya Uingereza kutekeleza sheria

Meya wa London, akisisitiza kuwa serikali ya Uingereza inapaswa kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai bila kusita kwa namna yoyote, alisema: "Wale wanaotuhumiwa kwa kufanya mauaji ya kimbari wanapaswa kuwajibishwa mbele ya sheria. Iwapo Netanyahu atasafiri kwenda Uingereza, nitaishinikiza serikali kuu kuhakikisha kuwa sheria za kimataifa zinatekelezwa. Wale waliofanya jinai za aina hiyo hawana nafasi mjini London."

Tel Aviv imejibu kwa ukali
Kuunga mkono kwa wazi kwa Meya wa London uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ambao utawala wa Kizayuni unaupinga vikali. Ubalozi wa utawala wa Kizayuni nchini Uingereza, huku ukilaani matamshi ya Sadiq Khan, ulimtuhumu kwa kuvuka mipaka na misingi ya kidiplomasia.

Misimamo ya awali ya Sadiq Khan kuhusu Ghaza

Ripoti hiyo imeeleza kwamba; wito wa kukamatwa kwa Netanyahu ndio msimamo mkali zaidi uliowahi kutolewa na Sadiq Khan tangu kuanza kwa vita vya Ghaza.

Tangu kuanza kwa mapigano hayo, Sadiq Khan amekuwa akisisitiza mara kwa mara umuhimu wa kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa. Hapo awali pia aliitaka serikali ya Uingereza kufanya mapitio ya kina na kusitisha leseni za usafirishaji wa silaha na vifaa vya kijeshi kwenda kwa utawala wa Kizayuni. Aidha, alitoa wito wa kusitishwa mara moja na bila masharti mapigano huko Ghaza pamoja na kufunguliwa haraka njia za kuingiza misaada ya kibinadamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha