Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sheikh Issa Ahmad Qassim, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain, amelaani udhibiti wa mfumo tawala juu ya mali za wakfu wa Kiislamu, hususan mali na majengo ya wakfu yanayomilikiwa na taasisi za Mashia nchini Bahrain.
Yeye katika akaunti yake kwenye mtandao wa “X” alisema:
"Kwa sheria za kidunia za leo, mali za wakfu zinachukuliwa kutoka mikononi mwa mwaminifu na kuhamishiwa mikononi mwa msaliti; kutoka katika kuhudumia wema na uadilifu kwenda katika kuhudumia uovu na ufisadi; na kutoka katika mkono halali ambao mtoa wakfu ameuweka kusimamia mali ya wakfu, kwenda katika mkono ambao hauna haki ya kuwa na mamlaka juu yake, jambo hili ni kinyume na mwenendo wa Uislamu."
Maoni yako