Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Huweida Jabq, daktari na mwanaharakati wa kitamaduni kutoka Italia, katika kikao maalumu cha “Hija; Mahali pa Miadi ya Umoja” kilichofanyika Jumatano kwa juhudi za Majma' al-'Alami li-Taqrib al-Madhahib al-Islamiyyah, alisema: “Siku za Hija ni siku za mshikamano wa mataifa, jamii, makabila na tamaduni, kuzikomboa roho kutoka katika utumwa wa mwanadamu, kuzinyenyekesha nafsi zenye kiburi na majivuno, kusafisha roho na kurejea kwa Muumba wake bila ya kushikamana na mambo ya dunia. Na ni dunia gani hii! Mahali ambapo Shetani aliyelaaniwa hutumia aina mbalimbali za wasiwasi, ufisadi, maovu na matendo mabaya ili kuwateka wanadamu katika mtego wake, ili athibitishe kwa Mwenyezi Mungu kwamba mwanadamu ni kiumbe kisicho na thamani anayekiendesha kwa urahisi; lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaonya waja Wake waumini dhidi yake na amewawekea katiba, sheria na miongozo ili wasiingie katika mtego wake.”
Alieleza Hija kuwa ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameifanya siku hiyo kuwa ni kiungo kati ya Muumba na viumbe Wake, na pia kati ya wanaume na wanawake waumini duniani kote, na akaongeza:
“Mwenyezi Mungu ameifanya ziara ya Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa wajibu kwa wale wenye uwezo wa kuitekeleza.”
Mwanaharakati huyu kutoka Italia alisisitiza: “Siku hizi, kutokana na ugumu na gharama kubwa, tunashuhudia matatizo mengi katika utekelezaji wa Hija, bei za viza ambpo hapo awali ilikuwa bure, pamoja na hoteli zimeongezeka kutokana na usimamizi wa serikali. Serikali inaweka kodi kubwa kwa wamiliki wa hoteli na kuwalazimisha kuongeza bei, vivyo hivyo, kuongezeka kwa gharama za usafiri wa ardhini, baharini na angani kunabeba mzigo mkubwa wa kifedha juu ya mabega ya mahujaji, jambo ambalo limevuka uwezo wao wa kifedha na huenda likawazuia kutekeleza faradhi hii ya kidini. Zaidi ya hayo, vikwazo vya umri vimewekwa kwa wale wanaoruhusiwa kutekeleza Hija, ni nani kati yetu anayeweza kuhakikisha kuwa ataendelea kuwa hai katika miaka ijayo ili aweze kufanya ziara hii kubwa?”
Alisema kuhusu jambo hilo: “Sisi tunaamini kwamba masuala haya yanapaswa kuwasilishwa kwa serikali inayohusika na Hija, na tunataka mambo haya yachunguzwe na yarahisishwe pamoja na kupunguzwa kwa gharama za Hija ili Waislamu wote waweze kuifikia, tukizingatia ziara ya Arubaini ya Imam Husayn ibn Ali, tunashuhudia zaidi ya mahujaji milioni 20 bila ya hitilafu wala tukio lolote baya hata dogo, hata hivyo katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambako idadi ya mahujaji kwa shida huzidi milioni mbili na nusu, hutokea matukio mengi, wizi na unyanyasaji dhidi ya wanawake, hata ndani ya Masjid al-Haram wakati wa Tawafu, mahujaji pia hubaguliwa na kushughulikiwa kwa misingi ya utaifa wao na mengineyo.”
Aliongeza kuws: “Tunataka hali ya Hija ichunguzwe na mipango yenye athari itungwe na nchi za Kiislamu ili itekelezwe kwa vitendo, na kwa matokeo yake utekelezaji wa faradhi hii kubwa ya kidini urahisishwe, kwa sababu Hija pia ni wakati wa watu kukutana, kuzungumza na kubadilishana mawazo.
Maoni yako