Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Shahidi Sayyid Ali Khamenei amejibu istiftaai kuhusu “kupata mapato yatokanayo na michezo ya kompyuta na PlayStation”, ambayo tunaiwasilisha kwa wapenda mada hizi kama ifuatavyo:
Kupata mapato yatokanayo na michezo ya kompyuta na PlayStation
Swali:
Je, kupata mapato yanayotokana na michezo ya kompyuta na PlayStation kuna shubha au kuna tatizo la kisheria?
Jawabu:
Mas-ala hutofautiana, Ikiwa asili ya mchezo wenyewe haina mambo mabaya, na katika michezo ya watu wengi hakutatumika vifaa vya kamari wala kusiwepo kushinda au kushindwa kwa mfumo wa kamari, basi kimsingi hakuna tatizo, na mapato yanayotokana nayo ni halali.
Maoni yako