Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi Mudarresi, mmoja wa wanazuoni wa Iraq, katika hotuba aliyotoa mbele ya kundi la walimu na wanafunzi wa hawza za wanawake, alisisitiza kwamba; Qur’ani Tukufu imeeleza kwa uwazi nafasi ya mama katika jamii, hasa katika muktadha wa kuzungumzia hatua kubwa na nyeti za kihistoria za ubinadamu; kwa namna ambayo mazungumzo kuhusu mama yake Nabii Isa (as) yanatangulia kabla ya mazungumzo kuhusu yeye mwenyewe (as), na pia mazungumzo kuhusu mama wa Nabii Musa (as) yanahesabiwa kuwa mhimili mkuu katika kufafanua harakati ya Nabii Musa (as).
Akaendelea kusisitiza juu ya kuwa mhimili wa nafasi ya mwanamke na hasa mama katika jamii, na nafasi yake katika malezi sahihi kwa ajili ya kujenga viongozi wa Kiungu, vizazi vyema, na wasomi waumini na thabiti. Aidha, kwa kurejelea nafasi za kihistoria za mama waumini katika kulinda imani ya vizazi katika hali ngumu zaidi, alisisitiza umuhimu wa kurudia nafasi hiyo katika zama za sasa.
Ayatullah Mudarresi alibainisha kwamba; mwanamke muumini anapaswa kuweka nia ya kuwa chimbuko la kuundwa kwa jamii njema; kwa namna ambayo wanawake, kupitia elimu yao katika hawza kwa njia ya ana kwa ana au kwa njia ya kielektroniki, na kwa kuiga mifano ya wanawake bora kabisa katika historia ya Uislamu, waweze kutekeleza nafasi kubwa na majukumu mazito yaliyo juu yao.
Maoni yako