Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, hafla hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwashukuru wanafunzi wa shule mbalimbali za Fudiya walioweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu, ili pamoja na kuwapongeza pia kuimarisha motisha na ari yao. Mwaka huu ulikuwa ni mzunguko wa kumi na tano wa kuandaliwa kwa hafla hii ya kiroho na kidini. Hafla ya mwaka huu iliangukia katika siku za muongo wa Karama, na ilifanyika tarehe 2 May 2026 katika mji wa Kano.
Katika sehemu nyingine ya programu hii, picha za wanafunzi wa shule ya msingi ya Minab zilionyeshwa ili kuenzi kumbukumbu yao; kwa kuwa walikuwa rika moja na mahufadhi hawa wa Qur’ani. Hatua hii pia ilifanyika kwa lengo la kuonesha na kulaani uhalifu na vitendo vya kigaidi vya serikali ya Marekani na Wazayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kabla ya kufanyika kwa hafla, wanafunzi hao waliohifadhi Qur’ani walifanya ziara ya kumtembelea kiongozi wa Harakati ya Kiislamu, Ibrahim Yaqoub Zakzaky. Alitoa pongezi kwao na kuwapa nasaha na maelekezo yenye thamani kuhusu kushikamana na Qur’ani Tukufu na kutekeleza mafundisho yake katika maisha yao ya kila siku.

Maoni yako