Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi al-Mudarrisi, katika kikao chake na kundi la walimu na wanafunzi wa Kitengo cha Utalii wa Kidini katika Chuo Kikuu cha Ahlul-Bayt (as), aliwataka Waumini kunufaika na mafunzo na mazingatio ya shule ya maisha, na kuyatumia katika kukabiliana na hali ngumu na changamoto zinazoukabili Umma wa Kiislamu.
Alisisitiza kwamba; Muumini hapaswi kujitosheleza tu na hisia za mshikamano au miitikio ya muda mfupi, bali anapaswa kujiandaa na kujitayarisha kwa kila tukio linaloweza kutokea.
Ayatullah al-Mudarrisi alieleza kwamba; Muumini anapaswa daima kuwa katika hali ya kujiendeleza kiroho, kisaikolojia na kiuchumi, na awe na maandalizi kamili katika nyanja zote.
Mwanazuoni huyo wa Iraq alisisitiza umuhimu wa kushikamana na dua sambamba na juhudi za kimada, na akaongeza: Waumini hawapaswi kujitosheleza tu na hatua za kimada, bali wanapaswa pia kujitahidi kwa dua ili kuleta usalama na amani kwa wote.
Maoni yako