Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kauli za hivi karibuni za Tom Barrack, balozi wa Marekani nchini Uturuki, kuhusu miundo ya utawala ndani ya Asia Magharibi, zimepata mwitiko mpana katika anga ya kisiasa ya nchi hiyo.
Barrack katika hotuba yake, kwa kutilia shaka ufanisi wa mifumo inayotegemea demokrasia na utawala wa sheria huko Uturuki na Asia ya Magharibi, alisisitiza kuwa; katika nchi nyingi za eneo hili, badala ya mifumo hiyo, mifumo inayotegemea uongozi wenye nguvu na uliokolea, na hata miundo ya kifalme, imeweza kuleta uthabiti zaidi.
Akiashiria mabadiliko yaliyotokea baada ya “Uamsho wa Kiislamu”, alidai kwamba juhudi za kuanzisha kwa haraka demokrasia ya Kimagharibi katika baadhi ya nchi zilisababisha kutokuwa na utulivu, vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuibuka kwa mifumo ya kiimla.
Katika kuendelea, Barrack aliitaja mifumo ya kifalme katika baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi kuwa mifano ya “uthabiti na ufanisi” ambayo, kwa mtazamo wake, imeweza kutoa usalama, ukuaji wa kiuchumi na kuboresha hali za maisha.
Pia, kwa kuisifu Israel kama “demokrasia yenye uhai” na kuitaja Uturuki kama mfano wa “uongozi uliokolea”, aliipa mifumo hii uzito katika kulinganisha na nchi nyingine za eneo; kauli ambazo zimefasiriwa na wakosoaji kama matumizi ya viwango viwili na kupuuzia misingi ya kidemokrasia.
Katika sehemu nyingine ya kauli zake, pia alisema kuwa “mataifa yenye nguvu ya kitaifa katika eneo hili ni tishio kwa Israel”.
Kwa kujibu misimamo hii, Gökçe Gökçen, naibu mwenyekiti wa Chama cha Republican People (CHP), katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, alielezea kauli za balozi wa Marekani kuwa ni “za kibaguzi” na akasema kuwa; kauli hizi—ikiwemo msisitizo kwamba “mataifa yenye nguvu ya kitaifa katika eneo hili ni tishio kwa Israel” pamoja na kusifu mfumo wa kitaifa wa Kiothmani—zinapaswa kutathminiwa kwa pamoja. Pia, akakosoa ukimya wa maafisa wa serikali, na kuuchukulia ukimya huo kama ishara ya kuidhinisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Maoni yako