Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mufti Mukaram Qadri, msomi na mufti wa Kisunni nchini Pakistan, katika hafla ya kumuenzi Kiongozi Shahidi Ayatullah al‑Udhma Sayyid Ali Khamenei (ra) iliyofanyika katika mji wa Karachi, Pakistan, alisema: Leo tunaposema kwamba katika vita hii tumesimama upande wa Iran, makusudio si kuiunga mkono nchi moja tu, bali tumesimama upande wa imani na Uislamu.
Akiendelea na hotuba yake alisisitiza kwamba; hakuna tofauti ya msingi kati ya Shia na Sunni, na wale wanaochochea mgawanyiko kwa hakika wanazitia nguvu njama za maadui; kwa hiyo Umma wa Kiislamu unapaswa kuungana juu ya mambo ya msingi yanayowakutanisha.
Mufti Mukaram Qadri aliendelea kueleza: Kiongozi Mkuu Shahidi, Ayatullah al‑Udhma Sayyid Ali Khamenei, alikuwa amelenga kulilea taifa ambalo kwa muda mrefu lilikuwa likijiandaa kukabiliana na Marekani. Uwepo wa miji ya chini ya ardhi ya makombora nchini Iran unaonesha kwamba; maandalizi haya yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi. Leo ingawa kiongozi ameshauawa, lakini mwanawe, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, ameshika bendera hii, na yeye ndiye kiongozi wa Umma wote wa Kiislamu.
Aliongeza kuws: Leo tunaposema kwamba katika vita hii tumesimama upande wa Iran, makusudio si kuiunga mkono nchi moja tu, bali tumesimama upande wa imani na Uislamu.
Mufti Mukaram Qadri, akirejea shughuli za kuchochea mgawanyiko katika mitandao ya kijamii, alisema: Leo baadhi ya watu wa kimadhehebu wanaendesha kampeni kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Iran kwa kutumia propaganda hasi za kidini na wanajaribu kuchochea mgawanyiko; ilhali vitendo hivi kwa hakika vinainufaisha Marekani na Israel. Kwa hakika tukitazama kwa makini, hakuna tofauti kati ya Shia na Sunni na makundi haya mawili yamesimama bega kwa bega.
Aliendelea kusema: Imamu Bukhari pia amenukuu riwaya kutoka kwa wapokezi wa Kishia, jambo linaloonesha kwamba kwa mtazamo wake, Mashia pia ni watu wa imani. Hivyo basi, ikiwa Imamu Bukhari ana mtazamo huu, basi hakuna nafasi kwa kauli za watu wanaochochea mgawanyiko.
Mtaalamu huyu wa dini huku akiashiria elimu ya kalamu ya Kisunni, alisema: Miongoni mwa Ahlus‑Sunnah, kuna maimamu wawili wakubwa katika elimu ya kalamu; Abu Mansur Maturidi na Abu al‑Hasan Ash’ari. Kiakida Ahlus‑Sunnah ima ni Maturidi au Ash’ari, Maimamu hawa wawili walitaja misingi kama vile kumwamini Mungu, Mtume, Akhera, Malaika na kwamba kheri na shari vyote vinatoka kwa Mungu kuwa ni nguzo za imani, na Mashia pia wanaamini kikamilifu misingi hii yote.
Mufti Mukaram Qadri mwishoni huku akisisitiza umuhimu wa umoja, alisema: Wakati Mwenyezi Mungu katika Qur’ani anamwamuru Mtume awaite Ahlul‑Kitab kwenye neno la pamoja, yaani Tawhidi na kujiepusha na ushirikina, basi kwa nini sisi, licha ya tofauti za madhehebu, tukusanyike juu ya yale tunayoshirikiana? Moto huu wa mgawanyiko umechochewa na watu wa kimadhehebu kwa maslahi yao binafsi. Leo ni lazima tusimame upande wa Iran, kwani ni sawa na kusimama upande wa imani.
Maoni yako