Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika kipindi nyeti cha kisiasa ambacho Iraq inapitia, na katikati ya hali ya sasa ya nchi hiyo, mahojiano haya ya wazi yanafungua milango iliyokuwa imefungwa kuhusu yaliyo nyuma ya pazia la migogoro ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na Mfumo wa Uratibu. Suala hili halijazuiliwa tu katika ushindani juu ya kamati za “kiserikali” ambazo zimegeuka kuwa uwanja wa mivutano ya usimamizi, bali linaendelea hadi kilele cha mvutano wa kibunge kwa kukusanya saini rasmi za kuvifukuza vikosi vya kigeni na kufunga ubalozi wa Marekani, kama mwitikio dhidi ya ukiukaji wa mara kwa mara wa mamlaka ya taifa.
Katika mahojiano haya yaliyofanywa na tovuti ya “Al-Maaluma” na “Ahmad Shahid”, mbunge wa Iraq, ramani ya njia ya “awamu ya tatu” pamoja na masharti magumu ya kujiondoa kwa Nouri al-Maliki mbele ya harakati ya kambi ya upinzani ambayo inajumuisha zaidi ya wabunge 100 na inapinga kuongezwa kwa muhula wa uongozi wa Muhammad Shiyai al-Sudani, inafichuliwa. Wapinzani hawa wanatahadharisha juu ya “kuanguka kwa uchumi” na kupotezwa kwa damu ya mashahidi. Katikati ya vitisho vya kiusalama kutoka nyuma ya mipaka ya Syria na mkwamo wa uchaguzi wa rais ambao bado haujapatiwa suluhisho, tunakuletea maelezo ya njama na miungano inayochora sura ya hatua ijayo katika kukabiliana na “kelele za ndege za kivita” na tamaa za nguvu za kisiasa.
Swali: Bado baadhi ya kamati za kiserikali hazijapatiwa uamuzi, sababu ni nini?
Jibu: Ndiyo, zipo kamati za kiserikali (A) na (B) ambazo bado hazijaamuliwa wazi, ikiwa ni pamoja na kamati za uadilifu, mafuta na nishati, usalama na ulinzi, kilimo na mashahidi; kwa sababu zina uzito mkubwa wa usimamizi na athari ya moja kwa moja katika uwanja wa kisiasa katika hatua ijayo. Kamati za uadilifu, usalama na ulinzi, pamoja na mafuta na nishati, ni miongoni mwa kamati muhimu zaidi zinazoshuhudia ushindani wa kisiasa kutokana na umuhimu na nafasi yake katika kusimamia na kufuatilia mafaili ya kimkakati.
Swali: Je, mmeanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kufunga ubalozi wa Marekani mjini Baghdad?
Jibu: Ndiyo, tumeshanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kufunga ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, pamoja na kuvifukuza vikosi vyote vya kigeni kutoka nchini. Hatua hii imechukuliwa kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya Wazayunina Marekani dhidi ya vikosi vya usalama na Hashd al-Shaabi. Aidha, kuna juhudi za kupitisha sheria itakayolazimisha serikali kutofanya makubaliano yoyote na vikosi vya kigeni au Marekani bila idhini ya Baraza la Wawakilishi.
Swali: Mgogoro wa kuunda serikali umefikia wapi katika mvutano wa nguvu za kisiasa?
Jibu: Faili la kuunda serikali limecheleweshwa hadi kura ya kumchagua rais. Kushindwa kwa vyama vya Kikurdi kuafikiana juu ya mgombea mmoja wa pamoja wa urais kumezidisha mgogoro wa kuunda serikali. Kuna shinikizo la wabunge kwenye kuharakisha uamuzi kuhusu suala hili, na endapo hali ya sasa itaendelea, hakutakuwa na chaguo jingine isipokuwa kuelekea kwenye uwanja wa kitaifa kwa ajili ya kuchagua mmoja wa wagombea kushika wadhifa wa urais kupitia bunge.
Swali: Ukweli kuhusu kujiondoa kwa Maliki na hatima ya al-Sudani kwenye muhula wa pili ni upi?
Jibu: Ndiyo, suala la mkwamo wa kisiasa kuhusu wadhifa wa uwaziri mkuu lilijadiliwa siku chache zilizopita na mgombea wa nafasi hiyo, Bw. Nouri al-Maliki. Ameeleza utayari wake wa kujiondoa kwa sharti kwamba hakuna waziri mkuu wa zamani atakayegombea. Kuna mgawanyiko kati ya nguvu za kisiasa kuhusu majina yanayopendekezwa kwenye nafasi hii.
Swali: Je, kuna kampeni ya kukusanya saini za wabunge kupinga muhula wa pili wa al-Sudani?
Jibu: Zaidi ya wabunge 100, kwa sababu mbalimbali zikiwemo kuanguka kwa uchumi na hali ya usalama, pamoja na kupotezwa damu ya mashahidi wa Hashd al-Shaabi, wamepinga kuongezwa muhula wa waziri mkuu wa sasa, Muhammad Shiyai al-Sudani, na wametia saini zao.
Swali: Nafasi ya serikali na bunge katika kulinda mamlaka ya taifa dhidi ya mashambulizi ya Wazayuni na Marekani ni ipi?
Jibu: Mamlaka ya Iraq ni mstari mwekundu ambao haukubaliki kuvukwa au kukiukwa kwa namna yoyote. Baraza la Wawakilishi tayari limejadili ukiukaji na mashambulizi dhidi ya mamlaka ya Iraq, na limetoa mapendekezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali na za kuzuia kupitia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya yeyote anayevuruga mamlaka ya Iraq.
Swali: Je, kumetolewa onyo kuhusu harakati za kutiliwa shaka za Marekani katika ushirikiano na makundi ya kigaidi nchini Syria?
Jibu: Tumetoa onyo kuhusu madhara ya harakati za kutiliwa shaka zinazoongozwa na Washington kwa lengo la kuzusha fitna kupitia seli za kigaidi. Uhamishaji wa hivi karibuni wa magaidi 5000, wengi wao wakiwa raia wa kigeni, kwenda Iraq ni kama bomu la muda lililowekwa.
Maoni yako