Jumanne 10 Machi 2026 - 19:50
Faalih Alfaya'dh, Atoa pongezi kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran

Hawza/ Raisi wa harakati ya Hashdu-sha'bi ya Iraqi, ametoa pongezi kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyed Mujtaba Khamenei, kwa anuani ya kuwa Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kusema: Irani itaendeleza njia yenye nguvu.

Kwa mujibu wa huduma ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Fa'lih Alfaya'dh, Raisi wa Harakati ya Hashdu-sha'bi ya Iraqi, ametoa pongezi kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyed Mujtaba Khamenei, kwa anuani ya kuwa Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Alfaya'dh katika ujumbe wake amesema: Kwa thati kabisa tunatoa salamu zetu za pongezi kuzielekeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyed Mujtaba Khamenei, kama Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Luninga ya Almayadini imenukuhu taarifa hiyo kwa kusema: Sisi tunalipongeza Taifa la Irani kutokana na mshikamano, uthabiti na upangiliaji walio uonesha katika kumchagua Kiongozi huyu.

Katika ujumbe huo imeandikwa kuwa: Mshikamano wao unaonesha uthabiti wa dola, nguvu za mfumo, na umadhubuti wao katika kukabiliana na changamoto tofauti.
Alfaya'dhi vile vile aliongzea kwa kusema: Sisi tunaamini kwamba, Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza njia yake yenye nguvu na kuhifadhi utawala wao wa busara.

Chanzo: Fars

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha