Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad al-Qattan, mwanachuoni wa Kisunni wa Lebanon na rais wa Jumuiya ya “Qawluna wal-‘Amal” ya Lebanon, katika mkutano wa kisiasa na kielimu ulioandaliwa na Vituo vya Imam Khomeini (r.a.) katika mji wa Tarya (Biqaa Kaskazini), kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka ya kuuawa kishahidi makamanda mashahidi (Sayyid Abbas al-Mousawi, Sheikh Ragheb Harb na Imad Mughniyeh), chini ya anuani “Mkakati wa Ushindi katika Kumbukumbu ya Mashahidi Makamanda”, alisisitiza tena ahadi ya uaminifu kwa njia na malengo ya makamanda hao mashahidi na akasema: Kuuawa kwao kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu haukuwa mwisho, bali ni hamasa na nguvu kubwa zaidi kwa ajili ya kuendeleza mkondo wa muqawana.
Sheikh Al-Qattan katika hotuba yake alikumbushia kuwa; heshima kubwa waliyoipata makamanda hao, na mbele yao akiwa Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Muqawama, imo kwenye kuwa yeye ni shahidi aliye hai katika njia ya Quds na katika kuwatetea wanyonge wa Palestina na Lebanon; mtu ambaye kwa damu yake safi alithibitisha kwa walimwengu ukweli wa kauli na misimamo yote aliyokuwa akiieleza katika safari yake ya jihadi.
Aliendelea kusema; katika mhimili wa masuala ya ndani huku akisisitiza: Baadhi ya sauti zinajishughulisha tu na kuzungumzia kuvuliwa silaha muqawama, ilhali serikali hadi sasa haijafanya zaidi ya kutoa matamshi, na haijasimama kwa namna yenye ufanisi bega kwa bega na wananchi, wakimbizi na majeruhi ambao walitoa roho na makazi yao kwa ajili ya taifa.

Mwanachuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon alisisitiza: Serikali inayotaka kuchukua nafasi ya muqawama, ni lazima kwanza iwe na nguvu na uwezo wa kuitetea ardhi na wananchi, na iweze kusimama mbele ya adui asiyeshikamana na ahadi wala makubaliano yoyote. Uhalisia unaonesha kuwa adui wa Kizayuni kila siku, kwa uchokozi wake wa mara kwa mara, anakiuka vipengele vya makubaliano yanayoitwa “usitishaji mapigano”.
Sheikh Al-Qattan aliwataka maafisa wa Lebanon wazitake nguvu za kimataifa zinazotoa maagizo ya kuvuliwa silaha, kwanza kabisa, zimlazimishe adui huyu kusitisha uchokozi wake.
Mwisho, Sheikh Ahmad al-Qattan alisisitiza kwamba; uaminifu kwa kumbukumbu ya makamanda mashahidi hudhihirika katika kushikamana na chaguo la muqawama, akisema: Maadamu ardhi yote ya Lebanon katika eneo la kilomita za mraba 10,452 haijakombolewa, na hakuna nguvu ya kitaifa ya kuzuia yenye uwezo wa kuwatetea Walebanon wote bila kujali madhehebu, mielekeo ya kidini au vyama vyao, basi tunakataa kabisa suala la kuvuliwa silaha.
Maoni yako