Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Marzieh Hashemi, Katibu wa Tamasha la Kumi na Sita la Filamu za Wananchi la Ammar, katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza mjini Tehran, akirejea mabadiliko ya mtazamo wa dunia kuhusu sera za Marekani, alisema: hapo awali kauli mbiu ya “Kifo kwa Marekani” ilikuwa ikisikika tu ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini leo kauli mbiu hii inasikika kote duniani, na hata ndani ya Marekani yenyewe bendera ya nchi hiyo inachomwa moto.
Aliongeza kuwa: watu duniani wameamka kutoka usingizi wa kughafilika na wamegundua ni nani dhalimu wa kweli. Leo hata wananchi wa Marekani wanaelewa kuwa inaposemwa “Kifo kwa Marekani”, kinachokusudiwa ni sera dhalimu za viongozi wa Marekani; sera ambazo kwa misingi ya fikra za kibeberu zinataka kuyafanya mataifa mengine kuwa watumwa wao.
Hashemi, akieleza kuwa anajivunia kuwepo na kuishi ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisisitiza: ninajivunia kuwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na ninatumai tushuhudie kuangamia kwa Marekani na kudhihiri kwa Hadhrat Walii wa Zama (a.j).
Katibu wa Tamasha la Kumi na Sita la Filamu za Wananchi la Ammar, katika kuendelea na maelezo yake, huku akijibu maneno ya kipuuzi na matamshi ya kudhalilisha ya Rais wa Marekani dhidi ya hadhi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alisema: Trump amekosea vibaya. Kinywa chake ni kichafu, na hapaswi kujiruhusu kuzungumzia kuhusu Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Maoni yako