Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Muhammad Sa‘idi, katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 23 January 2026, zilizofanyika katika Muswalla wa Quds mjini Qum Iran, huku akiwapongeza waumini kwa sikukuu za mwezi wa Sha‘aban, alisema: Imam Husayn (a.s.) anasema:
“Ninakuhusieni kumcha Mwenyezi Mungu; kwani Mwenyezi Mungu amemdhamini yule anayemcha na kusema kwamba, atambadilishia hali yake kutoka katika kile anachokichukia kwenda katika kile anachokipenda, na atamruzuku pasi na kutarajia.”
Akizungumza kuhusu sababu ya ushindi wa taifa la Iran na kushindwa kwa maadui katika matukio ya hivi karibuni, alisema: Wataalamu wanaamini kuwa Jamhuri ya Kiislamu na taifa kubwa la Iran, chini ya shinikizo zito la madhalimu wa dunia, limeweza kuonesha kiwango cha juu kabisa cha ustahimilivu. Kiwango hiki cha shinikizo, ambacho kilikuwa cha kila upande, hakijawahi kushuhudiwa duniani. Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na wananchi walishirikiana bega kwa bega, na hatua hii ngumu kwa kiasi kikubwa imefikia hatamu. Ingawa athari za mgogoro huu bado zinaendelea, kuna mambo kadhaa muhimu ambayo hayapaswi kupuuzwa.
Malengo ya Wachochezi wa Ghasia
Lengo la kwanza: Kusababisha njaa
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi mjini Qum alisema: Lengo la kwanza la adui katika suala hili lilikuwa kuleta njaa. Katika ghasia hizi, moja ya malengo ya wachochezi ilikuwa maghala makubwa ya maduka. Kwa kuchoma bidhaa za msingi katika maduka na kusababisha matatizo katika usambazaji wa bidhaa hizi, hali ilifikia kiwango cha hatari.
Lengo la pili: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi
Alisema: Lengo kuu la ghasia hizi lilikuwa ni kumdhoofisha Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Maadui walitambua kwamba busara na uongozi mkuu wa mfumo uko mikononi mwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ambaye amesimama imara kama kizuizi cha utekelezaji wa malengo dhalimu ya Marekani. Uongozi wa Mapinduzi mikononi mwa Kiongozi Mkuu umewaogopesha maadui, na ndio maana kwa mbinu mbalimbali wanafuatilia lengo hili ovu la kimkakati.
Imam wa Ijumaa wa Qum alisema: Katika matukio ya hivi karibuni, mpango mkuu wa Marekani ulikuwa na mfano unaofanana na Venezuela. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliwafikishia maadui ujumbe mara nyingi kwamba Iran itajibu aina yoyote ya uvamizi kwa kuhusisha eneo lote katika mgogoro.
Alikumbusha kuwa: Wazayuni walikuwa wamepanga vita hivi na malengo yao maovu kwa miaka mingi, wakisubiri fursa mwafaka ya kuyatekeleza. Kupitia hatua zilizochukuliwa na serikali kutatua matatizo ya wananchi, na kwa wananchi wetu wenye utiifu kwa Wilaya na waliodhamiria kupinga fitna, wachochezi wa ghasia walipata mshtuko mkubwa na walirudi nyuma kwa namna iliyo wazi.
Imam wa Ijumaa wa Qum aliongeza kuwa: Yuleyule Mwenyezi Mungu aliyemlinda Mtume Mtukufu (s.aww) dhidi ya washirikina kwa utando wa buibui, ndiye pia mwenye uwezo wa kumlinda Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi dhidi ya maadui, na kuzikabili njama za Marekani mhalifu kwa kushindwa kukubwa.
Tahadhari ya Kudumu Dhidi ya Fitna za Adui
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatima Ma‘suma (s.a.) alisema: Wananchi waaminifu wa Iran na serikali inayowahudumia wananchi wajue kwamba adui mhalifu hataacha hila, njama na uchochezi wake. Hivyo, tahadhari hii inapaswa kuendelea daima kwa maandalizi kamili na kwa kulipiza kisasi kikali dhidi ya viongozi na vipengele vikuu vya fitna.
Taifa la Imam Husayn (a.s.) Halishindwi
Akiadhimisha mazazi ya Imam Hussein (a.s.) na Siku ya Walinzi wa Mapinduzi, alisema: Imam Hussein (a.s.) ni kiini cha mapenzi ya taifa la Iran na Waislamu wote, wawe Mashia au Masunni. Mfano wa mapenzi haya huonekana katika siku za Arba‘in, hususan katika matembezi ya Arba‘in. Kwa mujibu wa Shahidi Qasem Soleimani, sisi ni taifa la Imam Husein (a.s.). Taifa la Imam Husein halishindiki. Walinzi wa Mapinduzi ni nembo ya nguvu na heshima ya taifa la Iran.
Imam wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Uhusiano usiovunjika wa Mapinduzi ya Kiislamu na mafundisho ya Imam Husayn (a.s.) umelifanya taifa letu kuwa taifa la Imam Husayn (a.s.), taifa ambalo kwa msukumo wa Mapinduzi ya Ashura, limeanzisha harakati za kujitegemea na maandalizi ya kudhihiri kwa Imam wa Zama (a.j.).
Aliongeza: Kwa mantiki ya Imam Husayn (a.s.), kuishi maisha ya udhalili chini ya dhulma ni sawa na kifo, na kifo chenye heshima ni sawa na uhai. Kwa sababu hiyo, katika mapambano ya kiustaarabu na kihistoria, upande wa haki—yaani taifa la Iran kama taifa la Imam Husayn—unasimama dhidi ya ubeberu wa dunia kama Yazid wa zama hizi. Kwa kufuata viongozi wa Kiungu na kutokusalimu amri mbele ya madhalimu, leo taifa la Iran limekuwa alama ya ushindi na wokovu wa mataifa yaliyodhulumiwa. Kinyume chake, kuwatii madhalimu na kunyamaza mbele ya dhulma kunasababisha fedheha na adhabu maradufu duniani na Akhera.
Imam wa Ijumaa wa Qum alisema: Taifa la Imam Husayn (a.s.), kwa sifa kama kuwa na malengo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu, kulinda uhuru na heshima mbele ya madhalimu, na kujali masuala ya Waislamu na waliodhulumiwa, halitashindwa maadamu litashikamana na misingi hii na mafundisho yenye uhai ya Imam Husayn.
Khutba ya Kwanza: Umuhimu wa Taqwa katika Nyanja Zote za Maisha
Ayatollah Sa‘idi katika khutba ya kwanza alisema: Kama tunavyozingatia taqwa ya Mwenyezi Mungu katika mambo binafsi kwa kujiepusha na yaliyo haramu na kutekeleza yaliyo wajibu, vivyo hivyo tunapaswa kuzingatia taqwa ya Mwenyezi Mungu katika masuala yote ya kisiasa, kijamii na mengineyo.
Alisema: Mwenyezi Mungu katika Aya ya 11 ya Surat al-Fath anasema:
“Watakuambia mabedui walio baki nyuma: zimetushughulisha sisi mali yetu na ahali wetu, basi tuombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo katika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda..”
Imam wa Ijumaa wa Qum alisisitiza: Mtume Mtukufu (s.a.ww) alipata ushindi wa kimkakati kupitia Sulhu ya Hudaybiyya. Alipokuwa akirejea Madina, Mwenyezi Mungu alimuarifu Mtume (s.a.ww) kwamba alipofika Madina, baadhi ya Mabedui wa pembezoni mwa Madina na wanafiki waliokataa kushirikiana na wewe, watakapouona ushindi wako, watatoa visingizio na kuomba radhi, wakisema: Tuombee msamaha kwa sababu hatukuja vitani; familia na watoto wetu vilituzuia.
Akiashiria kwamba watu hawa walikuwa wanafiki kwa sababu walichosema kwa ndimi zao hakikuwa mioyoni mwao, aliendelea: Qur’ani inasema kwamba katika mambo yote mawili walikuwa wakisema uongo; walidanganya walipotaja familia kama kisingizio, kwa kuwa sababu halisi ya kutohudhuria kwao ilikuwa ni hofu ya vita na kifo. Pia ombi lao la toba na msamaha lilikuwa la kinafiki.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatima Ma‘suma (s.a.) alisema: Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume (s.a.w.) awaambie watu hawa kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu ni mlinzi wa mtu, atakuwa salama katika hali yoyote, na ikiwa si mlinzi wake, hata kuwa nyumbani hakutampa usalama. Kama Mwenyezi Mungu angependa, angewateketeza hata mkiwa majumbani mwenu. Na Mwenyezi Mungu akitaka kumpa mtu manufaa, hakuna anayeweza kuyazuia.
Akiongeza kuwa hofu, udhaifu wa imani, kutafuta starehe, kukwepa majukumu na dhana mbaya juu ya Mwenyezi Mungu vilikuwa sababu zilizowazuia wanafiki kushiriki katika safari hiyo, alisema: Washirikina walipoona ushindi walioupata Waislamu, kwa unafiki walijionesha kama waliotubu, lakini Aya hii ilifichua ukweli wao
Maoni yako