Jumatano 21 Januari 2026 - 22:30
Kuendelea kwa Uislamu kunategemea damu ya mashahidi

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Arif Hussein Wahidi, katika hotuba yake alisema: Kuendelea na kudumu kwa Uislamu kunategemea damu ya mashahidi, na taifa lolote ambalo liko tayari kujitoa mhanga na kutoa damu yake, hakuna nguvu yoyote ya kikoloni au ya kitwaghuti duniani inayoweza kulishinda.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kongamano la “Kuwaheshimu Mashahidi wa Uislamu” lilifanyika mjini Islamabad, Pakistan, kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni, viongozi wa kidini na kijamii, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka madhehebu mbalimbali.

Katika kongamano hili, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Arif Hussein Wahidi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika hotuba yake huku akitoa pongezi kwa uthabiti wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alisema: Njama zote za ubeberu wa kimataifa, zikiwemo Marekani na Israel, dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapo awali zimeshindwa, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, katika siku zijazo pia zitashindwa.

Akiendelea na hotuba yake, alikumbusha tena: Kuendelea kwa Uislamu kunategemea damu ya mashahidi, na kila taifa lililo tayari kujitolea na kutoa damu yake, hakuna nguvu yoyote ya kikoloni au ya kitwaghuti duniani inayoweza kulishinda.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan aliongeza: Nguvu za Kiislamu na za ukombozi duniani kote zimesimama pamoja na mataifa yaliyodhulumiwa, na madola ya kikoloni hayawezi kufanikiwa katika malengo yao maovu.

Mwisho wa hotuba yake, aliwakumbuka na kuwaheshimu mashahidi wa Muqawama wa Kiislamu, akiwemo Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Shahidi Ismail Haniyeh, na Shahidi Yahya Sinwar, na akatoa heshima zake kwao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha