Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Ahmad Al-Koumi, kiongozi wa kitengo cha vijana cha Harakati ya Hamas kutoka Ghaza, Jumatano tarehe 24 December, katika kongamano la kielimu la kimataifa lenye anuani isemayo “Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah; Alama ya Muqawama na Umahiri wa Uongozi”, lililofanyika kwa ushiriki wa wanafikra, wanazuoni wa Hawza na vyuo vikuu pamoja na wanaharakati wa kitamaduni katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu cha Razavi, alifafanua kwa kina vipengele vya kifikra, kiitikadi na vya uwanjani vya misingi ya muqawama wa Kiislamu, na akamtaja Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kuwa mfano wa kudumu wa uongozi wa kidini na wa kiakili katika ulimwengu wa Kiislamu.
Akiashiria mazingira magumu na mashinikizo ya kudumu dhidi ya mkondo wa muqawama, alisema: njia ya mapambano imepita katikati ya vitisho, vikwazo, mazingira ya kuzingirwa na mashinikizo ya kulazimishwa, na kusimama huku si mwitikio wa kihisia au wa muda mfupi, bali ni chaguo la makusudi linalotegemea kumuamini Mwenyezi Mungu na kutembea katika njia ya Imam na misingi ya Kiislamu. Muqawama ulichukua sura katika nyakati ambazo baadhi walidhani kuwa; mashinikizo yanaweza kuvunja azma ya mataifa, lakini uzoefu umeonesha kuwa, ukweli haurudi nyuma mbele ya vitisho.
Mwenyekiti wa kitengo cha vijana cha Harakati ya Hamas, akieleza kuwa, katika historia ya kisasa daima mifumo miwili ya kifikra imekuwa ikikabiliana, aliongeza: mfumo mmoja unategemea maridhiano, upotoshaji wa vyombo vya habari na kujisalimisha mbele ya madola dhalimu, ilhali mfumo mwingine umejengwa juu ya busara ya kidini, imani, misingi ya Ahlul-Bayt (a.s) na kusimama imara. Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kwa ufahamu kamili, alichagua mkondo wa pili na akaoyesha kuwa, Muislamu wa kweli anapaswa kufanya maamuzi kwa misingi ya akili, misingi ya kidini na mtazamo wa mbali, si kwa misingi ya hofu au mahesabu ya kimaada pekee.
Akisisitiza nafasi ya wanazuoni na viongozi wa kidini katika kuongoza mkondo wa muqawama, alisema: katika njia hii, si suala la utii wa kipofu, bali ni ufuasi wa ufahamu kwa uongozi wa kidini na wa kiakili. Shahidi Nasrullah alikuwa mfano halisi wa kiongozi aliyekuwa na umahiri mkubwa katika fiqhi na misingi ya kidini, na wakati huo huo akiwa na uwepo hai na wenye athari katika uwanja wa utekelezaji; hata katika mazingira magumu zaidi, ikiwemo kushuhudiwa kwa mashahidi miongoni mwa wenzake na mashinikizo makubwa ya adui, jina la Mwenyezi Mungu na njia ya kimungu havikutoka katika kiini cha maamuzi.
Al-Koumi, akibainisha kuwa, ukweli utabakia kuwa hai na unaendelea kukua, alisema: endapo katika baadhi ya vipindi wasiwasi uliojitokeza kuhusiana na baadhi ya miundo au hatua, hiyo ni dalili ya uhai wa mkondo wa muqawama. Ukweli uko katika muqawama, utakaso na ukuaji wa kudumu, na Mwenyezi Mungu daima yupo katika uwanja wa haki. Uzoefu wa muqawama nchini Palestina na maeneo mengine katika ulimwengu wa Kiislamu umeonyesha kuwa, usalama wa kweli hutokana na kusimama imara na hatua ya makusudi, si kutokana na maridhiano au kurudi nyuma.
Akiashiria mashinikizo ya kiuchumi, ya vyombo vya habari na ya kisaikolojia ya maadui, aliongeza: Adui alitumia zana mbalimbali—kuanzia vikwazo na kuzingirwa hadi vita vya habari na upotoshaji wa taarifa—kwa lengo la kudhoofisha ari ya mataifa. Kuongezeka kwa shinikizo la maisha na kuundwa kwa mazingira yasiyo ya kawaida kulikuwa sehemu ya vita hivi mseto; hata hivyo, muqawama hupata maana yake hasa katika mazingira haya.
Watu na mikondo ya kweli hutambulika katikati ya mashinikizo haya, na leo matunda ya kusimama huku yameanza kudhihirika wazi kwa mataifa ya Kiislamu.
Mwenyekiti wa kitengo cha vijana cha Harakati ya Hamas, akisema kuwa, Shahidi Sayyid Hassan Nasralluh alikuwa zaidi ya mtu mmoja au kamanda mmoja, alieleza: kwa haraka aligeuka kuwa hakika ya kifikra na ya vitendo kwa wapigania jihadi na watu huru wa ulimwengu wa Kiislamu. Ujasiri wake haukutokana na hisia za mpito, bali ulitokana na fiqhi, tafakuri ya kina, subira na uelewa sahihi wa hali ya zama; aliweza kuunganisha ujasiri na busara, subira na mipango madhubuti, na kutoa mfano adimu wa uongozi wa kidini.
Alitaja suala la Palestina kuwa ni suala la msingi na la kimungu, akasema: Palestina si suala la kisiasa au kijiografia tu, bali ni suala la kiitikadi na linalohusiana moja kwa moja na heshima ya mwanadamu. Shahidi Nasrullah alilifuatilia suala hili kwa mtazamo wa imani na alikuwa na yakini kuwa muqawama bila kuunganishwa na imani ya Wilayat al-Faqih na uongozi wa kidini hautazaa matunda; kwa mtazamo wake, faqihi na kiongozi wa kidini lazima awepo moja kwa moja katika uwanja na achukue jukumu la kuuongoza umma kwa vitendo.
Al-Koumi, akirejea uhusiano wa kina kati ya misingi ya muqawama na utamaduni wa Ashura, alisema: uhusiano na Imam Hussein (a.s) hauishii katika kusoma au kusimulia historia pekee, bali ni uhusiano wa moyoni, kihisia na wa vitendo. Katika njia ya muqawama, habari chungu na mashahidi huumiza nyoyo, lakini maumivu haya hayabadilishi ukweli; badala yake, huimarisha zaidi azma.
Akisisitiza kushindwa kwa adui mbele ya mkondo wa muqawama, aliongeza: adui aliingia uwanjani kwa kutumia fedha, kuzingira, vitisho na vita vya kisaikolojia, lakini alishindwa kufikia malengo yake. Licha ya fitina na magumu mengi, muqawama wa Kiislamu, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuamini imani ya watu, umevuka hatua ngumu na leo umegeuka kuwa ukweli uliothibitika katika hesabu za kikanda na kimataifa.
Mwenyekiti wa kitengo cha vijana cha Harakati ya Hamas alitaja jukumu la leo la Umma wa Kiislamu kuwa ni kuitambua haki na kusimama upande wake, akasema: kuwa Muislamu katika mazingira ya sasa kunamaanisha kusimama imara na kutorudi nyuma. Maamuzi hayapaswi kufanywa kwa misingi ya maslahi ya kimaada au mahesabu ya kiuchumi pekee, bali juu ya msingi wa imani, busara ya kidini na Wilayat al-Faqih. Kuunga mkono haki kuna gharama, lakini gharama hiyo ni bei ya heshima na utu wa Umma wa Kiislamu.
Alisisitiza kuwa: njia ya muqawama ni ngumu, lakini ni njia ya mashahidi. Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah hakuwa mtu wa kawaida, bali alikuwa historia na chuo cha fikra; na mapambano ya leo si kauli au dai tupu, bali ni ukweli ulio hai na unaoendelea. Mwishoni, alitoa shukrani kwa wapigania muqawama, hususan vijana wa Ghaza na wanaharakati wa Harakati ya Hamas, kwa nafasi yao muhimu wanayoitekeleza kwenye uwanja huu.
Maoni yako