Jumatatu 8 Desemba 2025 - 16:45
Makumbusho ya Lincolnshire Nchini Uingereza Yaandaa Maonesho ya Athari za Kihistoria za Kiislamu Kutoka Makka

Hawza/ Athari za kale za Kiislamu zilizo maalumu sana, ambazo hapo awali zilikuwa zinaoneshwa Makka pekee, hivi karibuni zimewekwa katika maonesho katika Makumbusho ya Scunthorpe mjini Lincolnshire, na zimewapatia fursa adimu wapenda historia na sanaa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, athari hizi za kale na maalumu za Kiislamu ambazo hapo awali zilikuwa zinaoneshwa Makka pekee, sasa zimeoneshwa katika Makumbusho ya Scunthorpe katika mji wa Lincolnshire, na hivyo kutoa fursa ya kipekee kwa wanaovutiwa nazo.

Miongoni mwa athari muhimu zaidi katika maonesho haya ni kufuli na ufunguo wa mahali panapojulikana kuwa ni nyumba ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.) na mahali alipokuwa akipumzika.

Athari nyingine iliyowekwa katika maonesho haya ni mojawapo ya vitambaa vya zamani sana ambavyo vilikuwa vinatandikwa juu ya jengo la Al-Kaaba.

Abid Khan, mmoja wa wasimamizi wa athari zilizohamishwa kwa ajili ya maonesho haya, alisema: vitambaa vingi kati ya hivi vimepambwa kwa urembo wa uzi wa dhahabu safi ya karati ishirini na mbili.

Waandaaji wa maonesho haya wamesema kuwa; kutembelea athari hizi katika Makumbusho ya North Lincolnshire kunapatikana kwa watu wa madhehebu na dini zote, na kunatoa fursa ya “kufungamano na historia, uzuri na ufundi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha