Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, onyo hili limetolewa wakati huu ambapo vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya watu wa Ghaza vinaendelea bila kukoma, na katika kipindi cha wiki saba zilizopita, Israel imekiuka usitishaji vita takribani mara 600.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Indonesia, Jordan, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki na Falme za Kiarabu, siku ya Ijumaa, walitoa tamko la pamoja wakieleza wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na tangazo la hivi karibuni la jeshi la Israel la kufungua kivuko cha Rafah katika siku zijazo, lakini kwa namna ya kipekee kwa ajili ya kuruhusu tu kutoka kwa wakazi kutoka Ukanda wa Ghaza kwenda Misri.
Siku ya Jumamosi, mkutano ulifanyika Doha, ambao kimsingi ulikuwa ni kongamano la kidiplomasia. Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, Waziri Mkuu wa Qatar, ambaye pia alikuwa miongoni mwa wajumbe wakuu wa mkutano huo uliokuwa ukijadili usitishaji vita wa miezi miwili huko Ghaza, alielezea hali ya sasa kuwa ni “wakati nyeti”.
Alisema: “Hatuwezi bado kuuita huu kuwa ni usitishaji vita. Usitishaji vita hutokea pale ambapo vikosi vya Israel vinajiondoa kikamilifu na utulivu unapatikana Ghaza.”
Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nchi za Kiarabu zilisistiza kwamba Marekani inapaswa kutoa maelezo zaidi kuhusu mpango uliopendekezwa wa kujitawala kwa Wapalestina, na kuufafanua vyema kabla ya kura zaidi kupigwa; jambo hili limesababisha kushindwa kwa juhudi za Israel za kuzuia hatua hiyo.
Pia, kuna taarifa za mashambulizi makali ya makombora ya mizinga na moto mzito wa ndege za kivita katika maeneo ambayo kwa sasa jeshi la Israel limejikita mashariki mwa Khan Yunis na Rafah.
Vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya watu wa Ghaza tangia Oktoba 2023 hadi sasa vimesababisha kuuawa kwa zaidi ya Wapalestina 70,125 na watu 171,015 kujeruhiwa, kupata ulemavu au kuumia vibaya.
Chanzo: Al Jazeera
Maoni yako