Jumapili 7 Desemba 2025 - 13:00
Kamati ya Elimu ya Ataba Abbasiyya, Yaitembelea Taasisi ya Elimu na Utamaduni wa Kiislamu nchini Iran

Hawza/ Wajumbe wa kamati ya elimu kutoka katika Ataba Tukufu Abbasiyya walihudhuria katika Taasisi ya Elimu na Utamaduni wa Kiislamu, na katika kikao cha pamoja na wakurugenzi na marais wa vitengo vya utafiti walijadiliana kuhusu uwezo wa kielimu na sekta za ushirikiano pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ammar Hilali, mkuu wa “Idara ya Masuala ya Maarifa ya Kiislamu na Kibinadamu” katika Ataba Tukufu Abbasiyya, pamoja na ujumbe wake walihudhuria katika Taasisi ya Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu, wakatembelea maonyesho ya kudumu ya taasisi hiyo na kushiriki katika kikao cha pamoja na baadhi ya marais wa vitengo vya utafiti.

Katika kikao hiki, baadhi ya wakurugenzi wa taasisi walielezea shughuli na uwezo wa utafiti, na wakazitambulisha nyanja za ushirikiano kati ya taasisi hiyo na Ataba Tukufu Abbasiyya. Baadaye, Sheikh Ammar Hilali kwa kuonesha furaha ya kuwepo katika taasisi hiyo, alielezea malengo ya safari yake kuja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alisema: Moja ya malengo ya safari hii ni mwaliko kutoka katika vituo vya kielimu na watafiti wa Kiirani kushiriki katika “Kongamano la Urithi wa Kielimu wa Karbala katika Karne ya Kumi na Mbili” na pia “Kongamano la Urithi wa Kielimu wa Basra”; makongamano ambayo kwa mtiririko yatafanyika katika miji ya Karbala na Basra.

Mkuu wa “Idara ya Masuala ya Maarifa ya Kiislamu na Kibinadamu” katika Ataba Tukufu Abbasiyya pia alielezea kuanzisha daraja la mawasiliano ya kudumu kati ya Kituo cha Maarifa cha Ataba Abbasiyya na vituo mashuhuri vya kielimu vya Iran, hususan Taasisi ya Elimu na Utamaduni wa Kiislamu ya Ofisi ya Tabligh ya Kiislamu ya Hawza ya Qom, kuwa miongoni mwa malengo ya safari hii.

Sheikh Hilali mwishoni alisisitiza kuwa: Kituo cha Maarifa cha Ataba Abbasiyya kiko tayari kwa aina yoyote ya ushirikiano wa kielimu na vituo vya utafiti vya Iran; ikiwemo katika sekta za kufufua urithi, kuchapisha majarida ya elimu ya Kiislamu na pia kushiriki katika makongamano ya kielimu yaliyotajwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha