Jumapili 23 Novemba 2025 - 23:20
Je, kuvaa nguo nyeusi katika siku za Fatimiyya ni makruh?

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu swali kuhusiana na hukumu ya kisheria ya kuvaa nguo nyeusi katika siku za Fatimiyya, (Siku ambazo watu wanaadhimisha kumbukizi ya kuuwawa kishahidi Bibi Faatimah as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika desturi ya Kiislamu na hasa katika madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s) kuilinda na kuiheshimu alama za dini, pamoja na kudhihirisha mapenzi kwa Familia ya Mtume (s.a.w.w) kuna nafasi maalumu. Mojawapo ya vielelezo vya heshima hii ni kuandaa majlisi za maombolezo na kudhihirisha huzuni katika siku za maombolezo. Katika mazingira haya, mavazi na rangi ya nguo, kama alama ya nje inayodhihirisha hali ya ndani ya mtu, inaweza kuonesha undani wa hisia na mapenzi kwa waumini.

Kwa misingi hii, swali limeulizwa kuhusiana na hukumu ya kisheria ya kuvaa nguo nyeusi katika siku hizi, ambalo limejibiwa na Ayatullah al-Udhma Khamenei, na linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo.

Swali:
Je, kuvaa nguo nyeusi katika siku za Fatimiyya ni makruh?

Jibu:
Kuvaa nguo nyeusi katika siku za maombolezo ya Familia ya Isma na Utwahara (a.s), kwa ajili ya kutukuza alama ya Mwenyezi Mungu na kudhihirisha huzuni na majonzi, kunayo thawabu na malipo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha