Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ghaza limeibua hisia pana katika uwanja wa Kanda ya Morocco; kuanzia kulaani mpaka wasiwasi mzito, wakati ambapo maandamano ya mitaani katika eneo hili dhidi ya mauaji ya kizazi yanayofabywa na Wazayuni bado yanaendelea.
Kupitishwa kwa mswada wa azimio la Marekani kuhusu Ghaza na Baraza la Usalama kulitokea katikati ya jinai zinazoendelea za Wazayuni dhidi ya watu wa Ghaza na Palestina, na kufuatia kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kusimamisha mauaji haya ya kizazi na kuteketezwa watu wa Ghaza.
Kupinga Ukiritimba wa Kimataifa
Mu‘ād al-Jahri, mmoja wa viongozi wa Jukwaa la Maghreb linalounga Mkono Palestina na Kupinga Uhusiano wa Kawaida, katika mahojiano na tovuti ya habari “Al-Ahd Al-Ikhbari”, alisema: Jukwaa hili, pamoja na vipengele vya harakati za kupinga uhusiano wa kawaida nchini Morocco, limekataa azimio la Baraza la Usalama kuhusu mswada wa Marekani unaohusiana na Ukanda wa Ghaza.Akaongeza kuwa; Jukwaa hili limesisitiza kwamba azimio hilo linajaribu kupangilia upya hali ya ndani ya Ghaza kwa namna inayotumikia ajenda ya Kizayuni.
Al-Jahri aliendelea: Jukwaa hili limetangaza msimamo wake wa kupinga azimio hilo na kuliona kuwa halina kiwango kinachohitajika cha uwajibikaji; azimio ambalo halioneshi ukubwa wa jinai zifanywazo na wavamizi huko Ghaza wala kujibu haki za kisiasa na kibinadamu za taifa la Palestina.
Akaongeza: Pia, sisi katika Jukwaa tunapinga aina yoyote ya ukiritimba au uingiliaji kimataifa katika Ukanda wa Ghaza, kwa kuwa jambo hilo linaharibu mamlaka kamili ya ardhi ya Palestina na ni jaribio la kuanzisha ukweli mpya baada ya kushindwa kwa mkoloni kufikia malengo yake kwa kutumia nguvu.
Kiongozi mwandamizi wa Jukwaa la Morcco alisisitiza: Jukwaa hili linaamini kuwa suala la muqawama na silaha zake ni suala la ndani na la kitaifa kwa Wapalestina, na halipaswi kuunganishwa na mpangilio wowote wa kimataifa au kufanywa chombo cha shinikizo la kisiasa, kwani muqawama ni haki halali ya mataifa yaliyokaliwa kimabavu.
Akaeleza: Leo, kinachohitajika ni kusitishwa kwa vitendo mauaji ya kizazi, kuanza ujenzi upya bila masharti ya kubanwa, na kufanya juhudi kumaliza ukaliaji wa Kizayuni na kuwawezesha Wapalestina kutekeleza haki yao ya kujitawala na kuanzisha taifa lao huru lenye mji mkuu Jerusalem.
Jukwaa hilo hapo awali lilisisitiza katika taarifa yake kwamba; nguvu yoyote ya kimataifa iwapo itakuwepo basi jukumu lake lipunguzwe tu katika kusimamia usitishwaji wa mapigano mipakani chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, bila kupewa mamlaka au uwezo wowote wa kuingilia masuala ya Ghaza au kumpa mkoloni nafasi za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja.
Jukwaa hilo limeeleza kuwa; hali mbaya ya kibinadamu inahitaji kuharakishwa kufunguliwa kwa njia za kupitisha misaada na kuingia kwa misaada bila masharti yoyote au vizuizi, na kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa, hususan UNRWA, yaruhusiwe kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Jukwaa la Maghreb la Kuunga Mkono Palestina na Kupinga Uhusiano wa Kawaida lilisisitiza kuwa; watu wa Morocco watabaki thabiti katika kuunga mkono taifa la Palestina na watapinga kila aina ya uhusiano wa kawaida na utawala wa Israel unaopeana kinga kwa jinai za mkoloni.
Hatari zaidi kuliko Azimio la Kuigawa Palestina
Nchini Tunisia, vyama kadhaa vikiwemo “Chama cha Mwelekeo wa Umma” vililaani azimio hili. Muhsin al-Nabti, msemaji wa Mtazamo wa Umma, katika mahojiano na “Al-Ahd”, alisema: “Azimio la Baraza la Usalama namba 2803, huenda likawa hatari zaidi kwa Palestina na mustakabali wa suala la Palestina kwa ujumla kuliko hata azimio lenyewe la kugawa Palestina.”
Akaongeza: “Azimio hili ni la maafa, na likitekelezwa — jambo ambalo linatarajiwa — litakuwa mwisho wa kusikitisha wa kipindi kizima. Azimio hili ni hatari kwa Ghaza na Palestina, lakini kilicho hatari zaidi ni kwamba limetolewa katika mfumo ambao Syria imegeuzwa kuwa chini ya udhibiti wa Israel, na Lebanon iko katika hatihati ya kuporomoka kabisa; haya ni maeneo ambayo muqawama umeendelea kuwepo tangu kusainiwa kwa makubaliano ya Camp David na baada ya shambulio la Beirut, na ambayo yaliifanya muqawama imudu kusimama hata baada ya mikataba ya “amani” na Jordan na Oslo.” Alionya kuwa azimio hili ni “janga jipya kwa taifa la Palestina na umma wa Kiarabu.”
Maoni yako