Jumatano 19 Novemba 2025 - 22:47
Hotuba Kali ya Kocha wa Manchester City Dhidi ya Israel

Hawza/ Pep Guardiola, kocha wa Manchester City, kabla ya mechi ya misaada ya kibinadamu dhidi ya timu ya Palestina, alitoa hotuba kali dhidi ya jinai zinazofanywa na Israel huko Ghaza, na kuwalaumu viongozi wa dunia kwa kushindwa kuzuia mgogoro wa kibinadamu unaoendelea Ghaza.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, timu za Catalonia na Palestina zinatarajiwa kukutana Jumanne jioni katika uwanja wa Olimpiki wa Lluís Companys huko Barcelona. Tukio hili la michezo ambalo lilitangazwa na kampuni binafsi, limeungwa mkono na watu mashuhuri mbalimbali duniani katika nyanja za siasa na michezo, wakiwemo Guardiola. Mapato yote ya mechi hii yanatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ghaza.

Hapo awali, zaidi ya wanamichezo 70 wa kulipwa, akiwemo Paul Pogba, nyota wa zamani wa Manchester United, walitia saini tamko linaloitaka UEFA kuisimamisha timu ya utawala wa Israel kushiriki katika mashindano yake. Shirikisho la Soka la Ireland pia limeitaka bodi ya utawala ya soka Ulaya kuzuia ushiriki wa Israel katika mashindano yoyote mwezi Novemba.

Kabla ya mchezo kati ya Catalonia na Palestina, Guardiola alizungumza kuhusu mechi hiyo, vita na jinai za Israel Ghaza, na akasisitiza umuhimu wa kuwaunga mkono watu wa Ghaza huku akionesha kukosekana kwa hatua madhubuti kutoka kwa vyombo vikuu vya habari. Akasema: “Hii ni mechi maalumu. Leo kila kitu kiko wazi mbele ya macho ya watu wote, na kupitia mchezo huu Wapalestina wataona kwamba kuna sehemu ya dunia inayowafikiria.”

Akaendelea: “Dunia imewaacha Wapalestina peke yao. Sisi hatujafanya chochote kabisa. Hawana hatia kwa kuzaliwa huko. Sote tumeruhusu Israel kuwaangamiza watu hawa wote. Madhara tayari yameshafanyika na hayarekebishiki.”

Akasema pia: “Siwezi kufikiria mtu yeyote duniani anayeweza kutetea mauaji ya halaiki ya Ghaza. Watoto wetu wangeweza kuwa huko, na wangeuawa tu kwa sababu wamezaliwa mahali hapo. Nina imani ndogo sana na viongozi wa dunia wa leo, kwa sababu tunaona kuwa kwa ajili ya kubaki madarakani wanafanya lolote lile.”

Akaongeza: “Uwakilishi wa alama husaidia kuongeza uelewa wa jamii, lakini nyuma yake lazima kuwe na kitu – maana yangu ni msingi wa ukweli na uhai. Katika tukio hili, alama ni mechi ya mpira wa miguu, lakini tunachotaka kweli ni kwamba Wapalestina wahisi kuwa tuko nao kwa muda, na uwanja wao umejaa sauti za furaha na mshikamano wa watu.”

Chanzo: GIVEMESPORT

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha