Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Robo karne imepita tangia kuuawa kwake kishahidi kwa uonevu na katika hali ya upweke, shahidi Mahdi Eduardo Agnelli. Eduardo, kwa kuukubali Uislamu na kujiunga na madhehebu ya wokovu ya Ahlul-Bayt wa isma na utakaso (amani iwe juu yao), na kwa kufuata Mapinduzi ya Kiislamu, hakutengana tu na mkondo wa jadi wa familia yake, bali pia akawa ni alama ya muungano baina ya Italia na Uislamu safi wa Muhammad. Kwa uaminifu na ushujaa, alisimama dhidi ya shinikizo kubwa na hakukubali kuutoa kafara utambulisho wake wa Kiislamu na kimapinduzi kwa maslahi ya kimaada.
Kuuawa kwake kishahidi, kulikotekelezwa kwa mpango ulioratibiwa, bado kunazua maswali mengi. Nyaraka na ushahidi mpya zinaonesha kwamba kumuondoa katika nafasi ya urithi wa Fiat ilikuwa sehemu ya mradi mkubwa zaidi; mradi ambao usingeweza kuvumilia uwepo wa mrithi wa Kiislamu, huru na Mshia.
Kumbukumbu yake Eduardo leo hii ni kama mwanga ung'aao unaoangaza nyoyo na fikra. Yeye ni daraja imara kati ya mataifa na tamaduni; wito wa kimapinduzi wa kusimama dhidi ya dhulma na kuulinda ukweli na uadilifu.
Shahidi Eduardo Agnelli si jina tu katika historia, bali ni ukweli hai na wenye kuhamasisha; ukweli ambao nchini Iran na katika ulimwengu mzima wa Kiislamu umebaki kuwa alama ya muqawama, na nchini Italia unaweza kuwa mfano angavu wa kujikomboa kutoka katika minyororo ya utumwa mbele ya ubeberu wa kimataifa.
Maoni yako