Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge la Iraq (awamu ya sita tangu kuanguka utawala wa zamani), mwanasiasa huru, Abdulhadi Al-Hakim, ametangaza juu ya kukutana kwake na Ayatollah Al-Udhma Sayyid Ali Sistani.
Al-Hakim aliandika katika ukurasa wake wa Facebook:
“Alasiri ya Jumatano nilipata heshima ya kumtembelea Marjii wa kidini, Ayatollah Sistani, na kufaidika na miongozo, mawaidha, na dua zake. Yeye, kama ilivyo daima, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea kujitahidi katika kutetea haki za Wairaqi wanaodhulumiwa — watu walioteseka chini ya dhulma ya utawala wa zamani, na licha ya kupita zaidi ya miaka ishirini tangia kuanguka kwake, bado wengi wao hawajapata haki zao kikamilifu.”
Akaongeza kuwa pia alikutana na kufanya mazungumzo na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Muhammad Rida Sistani (mtoto wa Ayatollah Sistani), na wakabadilishana maoni kuhusu masuala ya sasa na mustakabali wa Iraq.
Kwa mujibu wa Al-Hakim, mawaidha na maneno haya ya Ayatollah Sistani yametolewa siku moja tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa bunge la Iraq, na yanaangazia umuhimu wa kulinda haki za wananchi na kuendeleza haki ya kijamii katika nchi.
Maoni yako