Jumapili 26 Oktoba 2025 - 00:10
Marehemu Naini alikuwa na mchango wenye athari kubwa katika uwanja wa siasa na jamii

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza alibainisha kuwa: “Ameonesha kwamba faqihi anaweza kufuatilia masuala ya kielimu na wakati huo huo awe na nafasi yenye athari katika uwanja wa kisiasa na kijamii.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanazuoni wa Iraq lilikutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Vyuo vya Kiislamu, kandokando ya pembizoni mwa kongamano la Kimataifa la Allamah Mirza Naeini.

Mirza Naeini — Alama ya akili mujahidi katika fikra za Kiislamu

Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Vyuo vya Kiislamu alivitaja vyuo vya kielimu vya Najaf na Qom kuwa ni vituo viwili muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu, akisema:
“Ushirikiano na mwingiliano kati ya hawza hizi mbili tukufu, Najaf na Qom, ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwenye kuinua hadhi ya Uislamu na Ushia. Mojawapo ya baraka za uendeshaji wa makongamano haya ni kuimarika kwa uhusiano wa karibu kati ya wanazuoni wa Iraq, Iran na nchi nyingine za Kiislamu.”

Ayatullah A‘rafi aliendelea kubainisha vipengele vya kielimu, kisiasa na fikra vya Allamah Mirza Naaini, na kwa kuashiria weledi na umakini wa mwanazuoni huyo wa jihadi katika kufuatilia mabadiliko ya zama alisema: “Nafasi yake katika kupambana na ukoloni wa Kiingereza, kutetea uhuru wa jamii ya Kiislamu dhidi ya wakoloni, na pia katika kuasisi fikra ya serikali ya Kiislamu ilikuwa muhimu sana.”

Akizungumzia mabadiliko ya kisiasa na kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu wakati wa Mirza Naeini, alisema: “Katika kipindi hicho nyeti, kutokana na uchambuzi makini wa hali na uelewa wa kina wa mazingira ya wakati wake, aliweza kuchukua misimamo iliyo wazi na ya kimkakati, ambayo ilibeba sura zote mbili — ya kielimu na kifaqihi, na pia ya kisiasa na kijamii.”

Ayatullah A‘rafi alisisitiza zaidi: “Marehemu Mirza Naeini, kwa mtazamo wake wa kina juu ya masuala ya zama zake, aliweza kuweka uwiano kati ya mafundisho ya kidini na mahitaji ya vitendo ya jamii, na akacheza jukumu muhimu katika kuiongoza jamii ya Kiislamu. Alithibitisha kwamba faqihi anaweza kujishughulisha na elimu na wakati huo huo kuwa na nafasi yenye ushawishi katika uwanja wa siasa na jamii.”

Leo, ushirikiano na muungano wa wanazuoni wa Iran na Iraq ni jambo lenye umuhimu mkubwa

Katika sehemu nyingine ya kikao hicho, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Naba’ al-Hammami — miongoni mwa walimu na watafiti wa hawza ya Najaf — akiipongeza ofisi ya Qom kwa kuandaa kongamano hilo la kimataifa la Allamah Mirza Naeini, alisema: “Kukifahamisha kizazi kipya na wanafunzi wa hawza juu ya nafasi ya kihistoria na wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya Ushia ni jambo muhimu sana.”

Akaongeza: “Leo hii, mwingiliano na umoja wa wanazuoni na wasomi wa Iran na Iraq ni muhimu mno. Kubadilishana maarifa na kunufaika zaidi na kazi za kielimu za hawza za Najaf na Qom ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwa kuimarisha utafiti na maendeleo ya kielimu katika vituo hivi viwili vya elimu katika dunia ya Ushia.”

Mwalimu huyo wa hawza ya Najaf pia alisema: “Kazi nyingi za kielimu za wanazuoni wakubwa wa hawza ya Najaf bado hazijachapishwa. Kuna haja kubwa ya kuchapisha na kusambaza kazi hizo bora na zenye thamani kwa wanazuoni, wanafunzi na watafiti.”

Hawza za Najaf na Qom, wabeba bendera wa madhehebu ya Ushia

Aidha, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hakim, mmoja wa walimu wa hawza ya Najaf, akitoa pongezi kwa hawza ya Qom kutokana na kuandaa kongamano hili la kimataifa, alisema: “Kumtambua Mirza Naeini na kazi zake ni jambo lenye thamani kubwa sana. Leo hii, ni muhimu wanafunzi wa elimu ya dini na watu kwa ujumla wawajue wanazuoni wakubwa wa hawza.”

Mwalimu huyo wa Najaf alibainisha: “Hawza za Najaf na Qom ni wabebaji wa bendera ya madhehebu ya Ushia. Kuna haja ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kielimu na kitamaduni kati ya hawza hizi mbili kuliko ilivyokuwa hapo awali.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha