Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Husayn Rafi‘ī, Naibu wa Tabliigh na Masuala ya Kitamaduni ya hawza, katika hafla ya kufunga kozi ya mafunzo na maelekezo ya "Karīmah Ahl al-Bayt (a.s.)" kwa wawakilishi wa shule za Amin na viongozi wa masuala ya tablighi katika mikoa, iliyofanyika katika kituo cha Yavarān Hadhrat Mahdī (a.f.) huko Jamkarān, alisisitiza umuhimu wa uangalizi wa kiroho kwa wahubiri, ikhlasi katika matendo na kujitakasa nafsi, akibainisha kuwa hitaji kuu la leo kwa Hawza ni “taqwa na maadili.”
Akimkumbuka Imam Khomeini (r.a.), mashahidi, majeruhi wa vita na wapiganaji wa kujitolea, alisema: “Mashahidi wana haki kubwa juu yetu, na tunapaswa kuendeleza njia ya Imam na mashahidi kwa umakini, ikhlasi na uadilifu wa kiroho, tujitahidi kutekeleza wajibu wetu kwenye kuendeleza njia yao kwa roho ya jihad na kumuabudu Mungu.”
Kozi ya mafunzo na maelekezo kwa viongozi wa uendeshaji wa tablighi na masuala ya kitamaduni kwa kuuzingatia maadili na kujilinda nafsi ndio ufunguo wa mafanikio ya wahubiri:
Naibu wa Idara ya Utabiri na Masuala ya Kitamaduni ya hawza, akibainisha kwamba kongamano hili ni kozi ya kumi ya mafunzo ya Karīmah Ahl al-Bayt (a.s.) na linahitimisha muongo mmoja wa shughuli za mafunzo na maelekezo kwa wahubiri, alisema: “Jambo la kwanza linalopaswa kuzingatiwa ni masuala ya kiroho, taqwa na kuilinda nafsi. Tunawasihi wote kwamba katika njia ya tablighi, zaidi ya yote, wajishughulishe na kujitakasa nafsi na taqwa. Leo zaidi ya wakati mwingine wowote, wanafunzi wa dini wanalihitaji hilo.”
Aliendelea kusema: “Ufunguo wa kutatua matatizo ya jamii na ya Hawza ni wa kimaanawi na taqwa. Kudhibiti matamanio ya nafsi na hisia binafsi, kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kujiepusha na kughafilika, ni msingi wa mafanikio ya wahubiri. Mhubiri anayepiga hatua katika njia ya jihad ya tablighi lazima awe katika ukumbusho wa Mungu daima, iwe ni katika upweke au mazingira magumu ya tablighi.”
Kutilia mkazo kushikamana na tauhidi katika kazi ya tablighi
Naibu wa Idara ya Utabiri na Masuala ya Kitamaduni ya hawza aliongeza: “Mhubiri anatakiwa aamini kwamba kazi hii inaendelezwa na dini ya Mwenyezi Mungu. Ni Mungu ndiye anaeleta athari, si sisi. Ikiwa imani hii itaimarika katika nafsi ya mwanadamu, kitendo chake kitakuwa cha kimungu na chenye athari. Maimamu wetu daima walikumbushia kwamba; mwanadamu ni fakiri, mwenye kuhitaji kwa Mungu. Imani hii ndiyo msingi wa harakati za mhubiri wa dini.”
Alisisitiza kuwa: “Matendo yetu yanapaswa kuwa juu ya msingi wa tauhidi na ikhlasi, si kwa kujionesha au kutafuta umaarufu. Kitendo kinachofanywa kwa ikhlasi kitabaki na kuwa na athari. Lakini kitendo kinachofanywa kwa nia ya kuvutia watu au kutafuta cheo cha kijamii, ni kinyume na mafundisho ya tauhidi na hakina matokeo.”
Ikhlasi na kutojulikana katika mwenendo wa Shahīd Qāsim Sulaymānī
Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Rafi‘ī, akiashiria mwenendo wa Shahīd Qāsim Sulaymānī, alimuelezea kama kielelezo cha ikhlasi na uangalizi wa nafsi, akisema:
“Shahid Sulaymani, licha ya kuwa kamanda mwenye mamlaka makubwa, daima alikuwa makini kujiepusha na kiburi. Imenukuliwa kuwa wakati mwingine baada ya vikao vya uongozi wa kijeshi, alikuwa akimwomba mwanachuoni aliyekuwepo azungumzie juu ya hasadi au kujiona bora. Alisema: ‘Leo wamenisifu kwenye kikao, ninaogopa nijione bora kuliko wengine.’”
Akaongeza kuwa: “Haj Qāsim alikuwa akipendelea kutojulikana. Wakati mwingine, walipokuwa wanataka kumheshimu kwenye kikao, walilazimika kumtafuta kwani hakuwa rahisi kumpata. Hiyo roho ya unyenyekevu na kujilinda nafsi ndiyo iliyomfikisha kwenye daraja tukufu la shahada na kulifanya jina lake libaki milele.”
Maoni yako