Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Gilan, mjini Rasht Irani, ikiwa na ujumbe maalumu kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kuhudhuriwa na maulamaa, viongozi wa kitaifa na kijeshi.
Tuzo hiyo ilitolewa kutokana na kutambua juhudi za Shirika hili katika kuwasilisha habari kwa ubunifu na kwa athari chanya, maarifa na mafundisho yanayohusu Swala, na mchango wake mkubwa katika kuimarisha na kueneza utamaduni mtukufu wa Swala ndani ya jamii ya Kiislamu.
Katika Hati ya Pongezi iliyoandikwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Hawza, na kutiwa saini na Ustadh Mohsen Qara’ati, Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Kusimamisha Swala, pamoja na Mohammad Hossein Rezaei, Mwakilishi wa Rais katika masuala ya Swala, imesemwa hivi:
Kwa salamu na heshima nyingi:
Taufiki ya kuhudumia Swala, nuru ya macho ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), ni hadia kuu ya Mwenyezi Mungu. Thawabu mnazozipata kupitia uungaji wenu mkono jambo la kusimamisha Swala ndio akiba bora kabisa, na fadhila mnazopokea chini ya kivuli cha Swala ndio bima iliyo bora zaidi.
Hivyo basi, kwa kutambua juhudi zenu zenye thamani kubwa katika kuwasilisha kwa ubunifu wenye athari habari na maarifa ya Swala, na kwa mchango wenu katika kukuza utamaduni wa nuru wa Swala ndani ya jamii, tunawasilisha shukrani na pongezi za dhati, kwa mujibu wa hadithi tukufu isemayo: “Asiyemshukuru kiumbe, hajamshukuru Muumba.”
Tunatarajia kwamba jitihada zenu zenye ikhlasi, zikiambatana na afya na ufanisi, zipokelewe na Mola Mtukufu.
Mohsen Qara’ati
Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Kusimamisha Swala
Mohammad Hossein Rezaei
Mwakilishi wa Rais katika masuala ya Swala.
Maoni yako