Jumamosi 11 Oktoba 2025 - 21:38
Israel na Trump Wamesalimu Masharti ya Muqawama Ghaza

Hawza/ Ayatollah Sayyid Yasin Musavi, akirejelea usitishwaji mapigano hivi karibuni Ghaza, aliutaja kama ishara ya kusalimu Israel na Trump mbele ya masharti ya Muqawama wa Kiislamu, na kusema kuwa Marekani ni “mama wa uovu katika eneo”.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Yasin Musavi, Imamu wa Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa wakufunzi wakuu wa Husseiniya ya Najafu Ashraf, alisisitiza kuwa:


"Tukio muhimu zaidi la hivi sasa duniani ni kusalimu Israel na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu, pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump, mbele ya masharti ya Muqawama wa Kiislamu huko Ghaza." Aliongeza kuwa usitishaji mapigano ulioanzishwa hivi karibuni ni “ushindi dhahiri wa Muqawama na matokeo ya kusimama imara kwa wananchi wa Palestina.”

Ayatollah Musavi katika khutuba zake za Ijumaa Baghdad alisema: “Kilichotokea leo ni matokeo ya miaka miwili ya Muqawama na kujitolea kubwa kwa wananchi wa Ghaza dhidi ya uvamizi wa Israeli; kipindi hiki kimesababisha zaidi ya mashahidi, majeruhi na wenye ulemavu 260,000.” Alisisitiza: kuanzishwa kwa usitishaji mapigano hakumaanishi kufungwa kwa kesi za uhalifu dhidi ya raia, bali ni wito wa kuwaadhibu wavamizi.

Imamu wa Ijumaa Baghdad, akiyalalamikia vikali matamshi ya Trump kwamba yeye ndiye aliyesababisha kusitishwa kwa vita, alisema:


"Yeye ndie aliyechochea mashine ya mauaji ya Israeli kwa silaha, misaada ya kisiasa na kufunikwa na vyombo vya habari, hawezi kuitwa mpatanishi wa amani. “Marekani ni mama wa uovu katika eneo na imempa Netanyahu mwanga wa kijani kuendelea na uhalifu huu.”

Alizilalamikia pia baadhi ya nchi za Kiarabu na Uturuki, akisema: “Nchi hizi ziliungana na Marekani na Israeli katika mazungumzo, lakini hazikuweza kuzuia mashambulio, bali kwa ukimya wao, kutokana na hofu ya kudumisha utawala wao nao walishiriki.”

Ayatollah Musavi aliongeza kuwa baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi zilipoona kuwa Marekani haikuwa tena mlinzi wa uhakika, zilianza kushirikiana na kuzungumza na Urusi, China na Iran. Aliongeza: “Mzunguko huu unaonesha kuwa mwisho wake wameelewa kuwa haifai kabisa kuitegemea Washingtoni japo ni kwa kuchelewa.”

Kuhusu vipengele vya usitishaji mapigano, Ayatollah Musavi alisema:

“Makubaliano yanajumuisha kurejea nyuma  sehemu ya wanajeshi wa Israeli na kuachiwa huru baadhi ya wafungwa wa Palestina,” lakini alionya kuwa hatuwezi kumwamini Netanyahu, kwani uvamizi unaweza kuanza tena wakati wowote. Alisisitiza: “Kuvunjwa kwa Hamas haikuwa sehemu ya makubaliano na Muqawama bado ipo imara kwa nguvu na silaha zake.”

Alisema kipimo cha ushindi si idadi ya mashahidi, bali kufanikisha malengo ya kimkakati. Aliongeza: “Muqawama umepata ushindi kwa kumlazimisha adui kutii masharti yake na kuondosha njama za kuuangamiza.”

Ayatollah Musavi, akiwashukuru viongozi wa Muqawama, alisema:

“Wamejitolea maisha yao kwa ajili ya uhuru wa taifa lao, huku Israeli, licha ya matangazo yake ya vyombo vya habari, ikiendelea kushindwa kimaadili na kimkakati.”

Katika sehemu nyingine, alitoa tahadhari kuhusu mradi wa “Mashariki ya Kati Mpya”, mradi unaolenga kugawanya nchi za Kiarabu na kupanua ushawishi wa Israeli katika eneo hili na akasema: “Marekani bado inaendelea kuitumia Israeli kuendeleza vita na machafuko.” Aliongeza pia: “Njia pekee ya kukabiliana na mpango huu ni kuegemea nguvu na umoja wa nchi za eneo.”

Mwisho, Imamu wa Ijumaa wa Baghdad aliwahimiza Waislamu na nchi za Kiarabu kuimarisha ushirikiano na kujenga nguvu huru dhidi ya ushawishi wa Marekani. Alisema: “Iwapo sisi Waislamu na Waarabu tungekuwa wamoja, si Trump wala mtu mwingine angekuwa na ujasiri wa kulazimisha masharti yake, na Israel isingeweza kumuua hata mtoto mmoja Ghaza."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha