Jumatano 8 Oktoba 2025 - 11:06
Ayatullahul-‘Uzma Jawadi Amuli: Jamii inaongozwa na maadili, si kwa elimu pekee

Hawza/ Mtume Mtukufu (saww) pamoja na kuwa na elimu pana, alisifiwa kwa sababu ya maadili yake adhim; kwani jamii inaongozwa na maadili, si kwa elimu pekee. Watu waliongozwa na mwenendo wa Mtume, si kwa elimu yake. Mwanachuoni wa kweli ni yule anayewalingania watu kimyakimya kuielekea haki kwa maadili mema.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amuli katika darsa ya wazi ya Fiqh, aligusia mada ya “Kemia iitwayo maadili", ambayo inawasilishwa kwenu kama ifuatavyi.

Angalieni sifa zote hizo alizokuwa nazo Mtume mtukufu; Mwenyezi Mungu Subhānahu wa Ta‘ālā alimpa elimu ya wa mwanzo na wa mwisho.

Lakini pamoja na elimu na nguvu zote hizo, kilichopewa kipaumbele ni tabia yake:


«إِنَّکَ لَعَلی‏ خُلُقٍ عَظیمٍ» 

“Hakika wewe uko juu ya maadili adhimu.”

Jamii inaongozwa na maadili; elimu bila maadili ina mipaka.

Hebu fikiri kwamba wewe ukawa ‘Allāmah, muhakkik (mtafiti), au Shaykh Tusi:

Wanafunzi wangapi wabobezi watanufaika nawe?

Watu wangapi katika jamii watanufaika na elimu yako?


Jamii inanufaika na maadili na mwenendo wako, si elimu peke yake.

Mtume naye alikuwa vivyo hivyo; watu hawakuwa wakiijua elimu yake, lakini walinufaika na tabia na mwenendo wake.

Ikiwa mtakuwa  «کونوا دُعاةً لِلنّاسِ بِغَیرِ ألسِنَتِکُم» “Walinganiaji wa watu bila kutumia ndimi zenu,” na mkaongoza kwa maadili, basi mtaweza kuhifadhi na kuongoza jamii, mfumo na umma.

Dars ya wazi ya Fiqh – Kitabu cha Ndoa, kikao cha 29; Tarehe: 25/09/1394 (Hijria Shamsiya)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha