Ijumaa 3 Oktoba 2025 - 20:33
Kwa nini uongo na kiburi hiki chote?

Hawza / Ulimwengu umejaa uzuri, mpangilio na nuru. Hata hivyo, mwanadamu kwa kujikita katika sura ya nje, kuchanganyikiwa kwa mawazo, na kusema uongo, anavuruga njia ya kimaumbile (fitra) na uwezo aliotunukiwa. Kiburi na ubinafsi humtenga na ukweli na uja, ilhali wanadamu wote ni wenye uhitaji, na Mwenyezi Mungu yuko juu ya kila udhaifu na upotofu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Marehemu Allāmah Hasan Zādah Āmulī katika moja ya hotuba zake alizungumzia mada ya “Muonekano wa mwanadamu aliechanganyikiwa huku asili yake ikihitaji uongofu”, ambayo inawasilishwa kama ifuatavyo:

Je, si hasara kwamba katika ulimwengu huu uliojaa uzuri wa kipekee, usafi na wema, mpangilio na ustaarabu, jamali na jalali — uzuri wa kipekee na nuru inayomiminika — sisi tunabaki kufunga fikra zetu tu katika sura za nje?

Ulimwengu huu wenye mwangaza mwingi, wenye viumbe mbalimbali, wa aina nyingi na waliosambaa kila kona, wenye nafasi na mienendo mingi — kwa nini tunabakia kupima mambo kwa mwonekano wa nje pekee?

Na viumbe vyote hivyo, nafasi zote hizo tunavifanya kama visivyo na uhai, kisha tunatoa hukumu kwa msingi wa sura ya nje?

Je, tumejionea vipi nguvu na uwezo mwingi aliotunukiwa mwanadamu unavyotumika? Kwa nia gani? Kwa dhamira ipi? Wakati huo huo, fikra na akili za mwanadamu zimepotoka, zimevurugika na kukosa mpangilio. Mikono yake inapeperushwa huku na kule, macho yake yanazunguka huku na kule, miguu yake inahama huku na kule — yote haya ni sura ya nje tu.

Sura ya nje inayolenga kucheza, kudanganya, na kusaliti.

Sasa tazama, nguvu na uwezo wake viko katika hali gani? Ubongo wake na chembechembe zote za uwepo wake zimevurugika, zimepinda, zimechanganyika na kukosa mpangilio; zimejaa mshangao na machafuko.

Ndiyo, mwanadamu anasema uongo, anasaliti. Uongo mmoja tu anaoibua na kuusema unatosha kuanzisha machafuko na vurugu zote hizi. Kila kitu kinatoka kwenye njia yake ya kimaumbile.

Kwa nini tunafanya hivi? Kwa nini tunasema uongo? Kwa nini tunazungumza kinyume na ukweli? Kwa nini tunasaliti? Kwa nini tunajifunga kwa kiburi na majivuno?

Nani ana haki ya kujivuna juu ya mwingine? Kiburi changu juu yako kina maana gani?

Sisi sote mwanzo wetu unajulikana, na mwisho wetu pia upo wazi. Sisi sote kwa hakika ni wanadamu wenye dhiki na uhitaji. Basi kiburi changu juu yako kina maana gani? Ni majivuno ya aina gani haya ambayo yamenishinda? Kwa lengo gani? Ni mzigo gani tunaojivika juu ya mabega yetu kwa kujiona na kujipenda kupita kiasi?

Na je, hali ya waja wa Mungu baada ya hayo iko vipi? Kasoro yao ni ipi? Wewe una haki gani ya kuwatendea wengine kwa namna hiyo?

Hata kama wanadamu wamepotea na kuzurura, hata kama ni washirikina — ni kipi kinachoweza kusemwa? Waangalie Namrūd na Firaun; walifikia kilele cha uchafu na upotovu, lakini bado Mola wao ni wa juu na mtukufu zaidi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha