Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mnamo Septemba mwaka 1960, Fidel Castro, kiongozi wa mapinduzi ya Cuba, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika hotuba ndefu zaidi na yenye kina katika historia ya taasisi hiyo, alikabiliana na ukoloni na ubeberu. Katika hotuba hiyo alisisitiza juu ya ulazima wa kung’oa “falsafa ya uporaji” ili kufanikisha amani ya kudumu, na akaonya kwamba muda wa kuwa falsafa ya vita imetanda duniani, hakuna taifa litakalofurahia uhuru na heshima.
Wachambuzi wanaamini kwamba leo hii maneno hayo hayo yamepata maana mpya kwa kuzingatia mgogoro wa Palestina. Yale ambayo Castro aliyaita “uporaji na unyonyaji”, hivi sasa yanaonekana katika miradi ya uvamizi na ujenzi wa makoloni ya walowezi ya utawala wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina; kuanzia kunyang’anywa vyanzo vya maji na uharibifu wa mashamba ya mizeituni, hadi mzingiro wa kiuchumi wa Ghaza na kugeuza mateso ya watu kuwa maabara ya majaribio ya kijeshi.
Castro mnamo mwaka 1960 alionya kwamba “mabeberu wote ni kitu kimoja na wote wameungana”, kauli ambayo leo hii imejidhihirisha katika msaada wa bila masharti wa Marekani na washirika wake wa NATO kwa utawala wa Kizayuni; msaada unaoambatana na kura ya turufu katika Baraza la Usalama na kuzuia mashitaka ya kisheria katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa.
Ripoti hii inaongeza kuwa: kama ambavyo Cuba katika miaka ya 60 ilikumbana na vikwazo, upweke na tishio la kuvamiwa, vivyo hivyo Palestina leo hii inakabiliwa na mzingiro wa kijeshi, njaa na uhamisho. Lakini kama vile Castro alivyopata jibu la shinikizo hizo katika “heshima, uhuru na mapambano”, ndivyo pia taifa la Palestina licha ya mauaji ya kimbari na uvamizi, limeendelea kuushikilia bendera ya muqawama na heshima.
Castro katika hotuba yake alisisitiza juu ya uadilifu kama msingi wa amani ya kudumu na akaonya: hakuna amani yoyote itakayofanikishwa kwa nguvu ya mabavu. Hivi sasa pia kuna juhudi za kuwalazimisha Wapalestina kukubali amani kwa msingi wa kusalimu amri na kuridhia uvamizi, lakini mapambano ya taifa la Palestina yanaonyesha kwamba mpango huu hauna mwisho wenye mafanikio.
Maoni yako