Jumanne 30 Septemba 2025 - 15:07
Kusisitizwa kuendelezwa kwa njia ya mashahidi

Hawza/ Kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin, hafla ya kumbukumbu imefanyika nchini Afrika Kusini kwa kuhudhuriwa na wahusika wa kisiasa na wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, sambamba na mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi makamanda wa mhimili wa muqawama, hafla ya kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Sayyid Hashim Safiuddin na kundi la viongozi wa muqawama, imefanyika katika Kituo cha Kiislamu cha mji wa Johannesburg huku ikihudhuriwa na wahusika wa kisiasa, wanaharakati wa kiraia, wawakilishi wa jumuiya zinazounga mkono Palestina na muqawama, pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afrika Kusini.

Katika hafla hii, wazungumzaji wakiashiria nafasi ya kihistoria ya viongozi wa muqawama katika kutetea malengo ya Palestina na kupambana na uvamizi, wameliheshimu kumbukumbu yao na kusisitiza kuendelezwa kwa njia ya mashahidi katika njia ya uadilifu, uhuru na kupambana na dhulma na uporaji.

Washiriki, kwa kusoma ujumbe wa mshikamano, wametangaza kuunga mkono muqawama wa taifa la Palestina na mataifa mengine yaliyo chini ya dhulma, na wakatoa wito wa mshikamano zaidi kwa mataifa kwa ajili ya kukabiliana na siasa za uvamizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa kibaguzi wa Kizayuni.

Katika hafla hii, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hotuba yake, sambamba na kuheshimu kumbukumbu ya makamanda na mashahidi wa mhimili wa muqawama, aliashiria athari ya kina ya fikra na mbinu za Sayyid wa mhimili wa muqawama, Shahid Sayyid Hassan Nasrallah, katika kuundwa kwa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Amefafanua uhalifu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa eneo na msaada usio na masharti wa Marekani kwa utawala huo, na akabainisha kuwa muqawama ndio njia pekee iliyo mbele ya wananchi wa eneo na ulimwengu kwa ajili ya kukabiliana na utawala huu.

Televisheni ya Afrika Kusini katika sehemu mbalimbali za taarifa zake za habari zilionesha mkusanyiko huu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha