Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi Sayyid wa mapambano ya Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrallah, mkutano mkubwa wenye anuani “Mashaahidi wa Umma” umefanyika katika mji wa Sargodha, Pakistan.
Mkutano huu uliandaliwa na Baraza la Wanazuoni wa Imamiyya Pakistan kwa kuhudhuriwa na wanazuoni, makhatibu, walinganiaji na shakhsia za kielimu na kidini kutoka miji na wilaya mbalimbali za jimbo la Punjab, Pakistan. Katika hafla hiyo, Sayyid Hassan Nasrallah alitukuzwa kama kielelezo kikubwa cha mapambano na uthabiti wa Umma wa Kiislamu.
Katika hotuba yake, Seneta Raja Nasir Abbas Jafari, Rais wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistan, huku akitukuza nafasi tukufu ya shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alizungumzia nafasi ya marjaʿiyya na mapambano katika historia ya kisasa ya Umma wa Kiislamu.
Marjaʿiyya daima ni chanzo cha heshima
Akasema kwa kusisitiza: Marjaʿiyya daima imekuwa chanzo cha heshima na utukufu wa taifa la Kishia, na mfumo huu ndio nguzo imara zaidi ya uongofu na uimara wa jamii yetu.
Mapambano; kinga dhidi ya ubeberu
Rais wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistan akielezea hali ngumu ambayo jukwaa la mapambano lilianzishwa, alisema: Mapambano yaliwekewa msingi katika mazingira magumu na tata zaidi, lakini si tu yalisalia thabiti, bali yaliweza kubadilisha mizani ya nguvu katika eneo. Leo pia kuwepo kwa jukwaa hili ni jambo la lazima na la kimaisha, na ni mstari huu wa mbele pekee unaoweza kuyaokoa mataifa dhidi ya njama za ubeberu wa kimataifa.
Sifa na shakhsia ya Shahidi Nasrullah
Aliendelea huku akitukuza upeo wa shakhsia ya kiongozi wa Hizbullah Lebanon na kusema: Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah alikuwa taswira ya azma, ikhlasi na unyenyekevu. Ujasiri, taqwa, zuhudi na maadili yake ya juu vilimfanya awe sura ya kipekee miongoni mwa viongozi wa kisasa.
Matarajio ya mustakabali wa mapambano
Seneta Raja Nasir Abbas Jafari akirejelea urithi wa kudumu wa shahidi Nasrullah alisisitiza: Yeye aliiandaa Hizbullah si kwa ajili ya mazingira ya sasa pekee, bali pia kwa kukabiliana na changamoto za baadae. Kwa hivyo, katika madhehebu ya mapambano hakuna nafasi ya kukata tamaa. Sasa kuliko wakati mwingine wowote, tunapaswa kuwa na matumaini kwa mustakabali na kuendeleza njia ya mapambano kwa azma na mshikamano.
Mashahidi ni dhamana ya uhai wa mataifa
Mwisho alisema: Ukuu wa mashahidi ni uhai wa mataifa. Ni wajibu wetu kwa mshikamano, basira na ustahimilivu, kuhuisha njia yao na kuendeleza mwenge wa mapambano kizazi hadi kizazi.
Hafla hii ilihitimishwa kwa kusomwa Fatiha na dua ya pamoja kwa ajili ya kuienzi roho ya shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na mashahidi wengine wa mapambano na Umma wa Kiislamu.
Maoni yako